Huduma ya treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda Bara ilisimama kwa muda kadhaa kutokana eneo korofi baina ya stesheni za kilosa mkoani Morogoro na Gulwe Mkoani Dodoma.
April 28 2016 taarifa imetolewa kwamba eneo hilo korofi limetengemaa hivyo Huduma ya usafiri wa treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda mikoa mingine kwa kutumia reli ya kati utaanza rasmi mei mosi mwaka huu.
Kusimamishwa kwa usafiri wa Treni ulisababisha abiria kupandia treni Dodoma badala ya Dar es salaam hivyo sasa treni ya kwanza ya Deluxe itaondoka kutokea Dar es salaam kwenda kigoma.
Post a Comment