Loading...

Watendaji K’ndoni watangaziwa kiama

Boniface Jacob, Meya wa Halmashauri ya KinondoniBONIFACE Jacob, Meya wa Manispaa ya Kinondoni amewatangazia kiama watendaji wa kata na mitaa ambao wanaihujumu serikali katika ukusanyaji mapato na kukwamisha shughuli za serikali, anaandika Pendo Omary.
Jacob ametoa kauli hiyo leo, wakati wa mkutano wake na watendaji hao, uliohudhuriwa pia na Ally Hapi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Kwa mujimu wa Jacob, mpaka sasa tayari watendaji watatu wamefukuzwa kazi na wengine watatu kusimamishwa kupisha uchunguzi kwa sababu ya kuhusika na kutuhumiwa kufuja fedha za maendeleo zinazotolewa na Halmashauri.
“Tayari wapo watendaji wa mitaa na kata waliochukuliwa hatua za kinidhamu. Watendaji wa kata waliofukuzwa ni; Ernest Missa, Ally Bwamkuu na Shabani Kambi yeye amesimamishwa. Watendaji wa mitaa waliosimamishwa ni; Dustan Kikwesha na Richard Supu huku Aneth Lema akifukuzwa,” amesema Jacob.
Jacob amesema watendaji hao wametuhumiwa kusababisha upotevu wa fedha zinazotolewa na Halmshauri zaidi ya Sh. 400 Milioni hali inayochangia kukwamisha maendeleo.
Wakati watendaji hao wakifukuzwa kazi na wengine kusimamishwa, Jacob amesema “kabla ya kumaliza mwaka wa fedha 2015/2016, tuna zaidi ya Sh. 60 Bilioni mitaani hazijakusanywa. Kuna watendaji wengine wanaona sio wajibu wao kuzikusanya.
“Kwa mfano mpaka sasa kata zinazoshika mkia kwa ukusanyaji duni wa kodi ya majengo ni; Mburahati Sh. 1,965,147 Milioni, Kibamba Sh. 1,832,150 Milioni, Mabibo Sh. 1, 824, 803 Milioni, Mabwepande Sh. 1,754,067 Milioni na Kimara Sh. 235,832. Kwa mtu ambaye hatusaidii kwenye jukumu hili tutamtafutia kazi nyingine ya kufanya,” amesema Jacob.
Aidha, amezitaja kata ambazo zimefanya vizuri katika ukusanyaji wa kodi ya majengo kuwa ni; Msasani Sh. 822,581,821, Sinza Sh. 518,136,560, Mikocheni Sh. 215,986,462, Mbezi Juu Sh. 116,170,484 na Bunju Sh. 86,772,400.
Kwa upande wake Hapi amesema “watendaji wetu wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea. Nimeamua kuisaidia Halmashauri ya Kinondoni. Afisa biashara tumemwondoa. Haendani na kasi yetu. Kuna watendaji wanawanyanyasa wananchi, wanawatoza fedha hawawapi risiti. Ninatoa onyo.”

China Wammwagia Sifa Rais Magufuli....Wasema Kaipaisha Tanzania Kimataifa

SERIKALI ya China imeiunga mkono serikali katika mkakati wake wa kutoa elimu bure, ikisisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, Tanzania inasifika duniani.

Katika kuunga mkono elimu bure, ubalozi wa nchi hiyo nchini umetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 28 kwa shule mbalimbali za msingi katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Balozi wa China hapa nchini, Dk Lu Youq’ng alisema msaada huo ni moja ya juhudi za nchi yake kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kutoa elimu bure. 

“Wakati mimi nimechangia madawati 300, Kampuni inayochimba madini hapa ya Sun Shine Group imechangia madawati 100 ili kuniunga mkono,” alifafanua.

Akikabidhi madawati hayo katika mikutano mitatu tofauti kwenye mji wa Kiomboi, Shelui na Misigiri, Balozi Youq’ng alisisitiza umuhimu wa Tanzania kuwekeza kwenye elimu kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli.

“Hata kama nchi ni maskini kiasi gani, lazima elimu itiliwe mkazo; tena iwe ni elimu bora na elimu bora haiwezi kuja kwa wanafunzi kukaa chini. “Madawati ni moja ya mambo ambayo yanamjengea mwanafunzi mazingira mazuri ya kujifunzia,” alisema.

Aliongeza, “kutokana na umuhimu huo, ndio maana mbunge wenu aliponijia na kuniomba msaada wa madawati, sikusita hata kidogo. Nilijua anafanya hivyo ili kuisaidia jamii yake kuboresha elimu”. Aliyeomba msaada huo ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Aidha, balozi huyo amewapongeza wakazi wa mkoa wa Singida kwa kumchagua Dk Magufuli kuwa Rais na kuongeza kusema kuwa chini ya uongozi wake sasa Tanzania inasifika duniani kote. “Nitahakikisha nchi yangu inaendelea kusaidia maendeleo ya nchi hii kwa kuwa urafiki wetu ni wa enzi na enzi,” alisema.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe alisema kuwa mkoa unathamini msaada huo kwa kuwa umepunguza kwa kiasi kikubwa upungufu wa madawati 4,016 ambayo wilaya hiyo ilikuwa nao.

BREAKING NEWS: BAADA YA SERIKALI YA MAGUFULI KUTUMBUA JIPU LA TANESCO MENEJA WA SHIRIKA LA UGAVI WA UMEME KUFANYA YAKE NA KUMKAMATA MBOWE KWA KULITIA HASARA SHIRIKA HILO YA ZAIDI YA SH.MIL.5O NA KUCHUKUWA HATUA HII.....

 
Pwani. Shirika la ugavi wa umeme (Tanesco) Mkoa wa Pwani limemkamata mmoja wa wamiliki wa eneo la maegesho ya magari la White Star Munira Mbowe kwa kosa la kujiunganishia umeme kinyemela.
Mbowe ambaye ni mmiliki wa eneo hilo lililopo Kiluvya kwa Komba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam alikamatwa jana baada ya kufanyika msako wa kushtukiza kwa wateja mbalimbali waliohisiwa kujiunganishia umeme.
Mmiliki huyo wa Yadi akiwa amejiunganishia umeme bila ya kufuata taratibu zozote za Tanesco ambapo ameisababishia shirika hasara ya zaidi ya sh. Mil. 50.
Akizungumza kwenye Yadi hiyo ,Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Henry Byarugaba alisema baada ya kufanya ukaguzi waliweza kukuta mteja huyo akiendesha shughuli zake kwa kutumia umeme huo na kuisababishia Tanesco hasara ya Sh 50 milioni.
"Tumekuwa tukibuni mbinu mpya kila kukicha ya kuwatia mbaroni wateja wetu wanaotuhujumu na leo ( jana) tumembana huyu anayedaiwa ni mmiliki wa Yadi ya White Star baada ya kukuta anatumia umeme uliotokana na kujiunganishia laini tatu za nyaya zinazopitisha umeme,” alisema Byarugaba
Byarugaba alibainisha kuwa kwa sasa Mbowe amefikishwa kituo cha polisi Kibaha na utaratibu mwingine unaendelea.
Alisema hii si mara ya kwanza kwa Mbowe kufanya hivyo kwani walipofanya msako mwaka jana walimkuta amejiunganishia umeme na alichukuliwa hatua.
Kwa upande wake Mbowe alijitetea kuwa hajui lolote kuhusu kuunganishiwa njia hizo tatu za umeme kwa sababu mara nyingi hufanya shughuli zake jijini Dar es Salaam na shughuli zake nyingi pia huzifanyia huko jijini na ni mara chache huja hapo Kibamba.
“Ni kweli tumekutwa na kosa na kuiba umeme lakini jamani nataka niwaeleze kuwa mimi sihusiki na kingine nawaomba msinitoe katika vyombo vya habari kwani haya ni maisha tu, sio vizuri kunitoa jamani mimi sihusiki kabisa katika wizi huu “ alijitetea Mbowe.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Taneso Pwani Selemani Mgwila alisema kitendo alichokifanya mteja wao huyo ni kosa kubwa kwani umeme waliokuwa wanatumia katika ‘yadi’ ulisababisha upotevu wa makubwa.

Mamlaka ya Mapato (TRA) Yataifisha na Kugawa Bure Sukari Mifuko 5,319 toka Brazil Yenye thamani ya Sh 373.5 milioni


Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Million 373.5  kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Million 246.

Kwa Hali Hii ni ‘Ni Ndoto Tanzania Kuwa na Uchumi wa Viwanda


Wabunge wamesema ni vigumu Tanzania kufikia lengo la kuwa na uchumi wa viwanda iwapo Serikali itaendelea kusuasua kutekeleza miradi yenye mchango mkubwa katika sekta hiyo.

Akisoma maoni ya Kamati ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka 2016/17, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Vicky Kamata alisema hawaridhishwi na namna Serikali inavyotoa fedha za bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.

“Kwa kuzingatia takwimu hizi ni dhahiri miradi mingi ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha haitatekelezwa,” alisema Kamata.

Alisema kamati hiyo inaunga mkono dhamira ya Serikali ya kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025 lakini hairidhishwi na kasi ya utekelezaji wa azma hiyo.

“Hali hii ikiendelea itakuwa vigumu Tanzania kuwa nchi ya viwanda iwapo Serikali itaendelea kuchelewesha utekelezaji wa miradi yenye mchango mkubwa katika sekta hii,” alisema.

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu alisema: “Kamwe tusijiaminishe kuwa tunaweza kufikia Taifa la viwanda kwa Sh42.159 bilioni kwenye bajeti ya mwaka kama fedha za maendeleo kwa ajili ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,” alisema.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti bungeni jana Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kati ya viwanda 106 vilivyofanyiwa tathmini, viwanda 45 vinafanya kazi, 24 vinasuasua na 37 vimefungwa.

“Mpango wetu ni kuhakikisha kuwa viwanda 35 vilivyobaki vinafanyiwa tathmini haraka na kabla ya nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha unaoanza Julai Mosi mwaka huu, hatima ya viwanda visivyofanya kazi itajulikana,” alisema.

Alisema hatima ya wenye viwanda visivyofanya kazi ni kwa wamiliki kutekeleza mkataba ya mauzo au kupewa wawekezaji wapya ili waviendeleze,” alisema.

Wizara hiyo imeomba kutengewa Sh 81.87 bilioni katika mwaka wa fedha 2016/17 kati ya hiyo, Sh41.87 bilioni sawa na asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh40 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Mama Salama Amtetea Rais Mstaafu Jakaya Kikwete


SALMA Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ameonesha kukerwa na wale wanaoshambulia utawala wa mumewe (Rais Kikwete) na kwamba, hakuna sababu ya kufanya hivyo.

Mama Salma alisema hayo jana kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) unaofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu.

Alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kujitokeza hadharani kumkingia kifua mtoto wake Ridhiwani Kikwete kuhusu kuhusika kwake na mkataba wenye utata wa Kampuni ya Lugumi.

“Kila mwaka naendelea kuisemea serikali iliyopo madarakani mambo mazuri, acheni hali ya kukaa na kuanza kusema kwamba serikali ile ilikuwa vile na serikali hii iko hivi.

“Wala msisema yule alikuwa vile na huyu yuko hivi, kwa kumalizia hayo napenda kusema mume wangu ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa anawasalimia sana,” alisema Mama Salma.

Akizungumzia utumbuaji wa majipu alisema, serikali kwa sasa imeanza kutumbua majipu makubwa kuanzia juu lakini zipo taarifa kuwa, yapo majipu mengine ngazi za chini pia ndani ya CCM.

Alisema, “kila anayejitambua kuwa ni jipu kabla hajafikiwa ni bora akajitumbua mwenyewe au ajipake spriti ili jipu hilo lipoke mapema kabla halijatumbuliwa.”

Hata hivyo alionesha wasiwasi kuwa, kuna uwezekano miradi mingi ya UWT ikachukuliwa kutokana na umoja huo kuwa na mali ambazo zinaonekana kumilikiwa bila kufuata taratibu.

Alisema, kwa upande wa ardhi kuna viwanja vingi ambavyo havina hati na vimekaa muda mrefu bila kuendelezwa jambo ambalo kwa sasa mameya wanaweza kuvibadilishia matumizi.

BREAKING NEWS: TAARIFA KUTOKA IKULU RAIS MAGUFULI KUTOA TAMKO KALI KWA WATUMISHI WAUMA KUWA HATOWAVUMILIA WATAKAO JIHUSISHA NA VITENDO VYA UFISADI NA RUSHWA HUKU AKISEMA KUWA ATAWATMBUWA MPAKA MWISHO WA DUNIA NA KUSEMA HAYA.....


 
Rais Magufuli amerejea kauli yake kuwa serikali yake haitawavumilia viongozi na watumishi wa umma ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, huku akisema ataendelea kutumbua majipu kwa yeyote atakayebainika kuchezea mali za umma ili kulinda maslai ya wengi, hususani watanzania wanyonge.

"Ninafanya kwa niaba yenu, ninafanya kwa niaba yenu, ningekuwa sifanyi kwa niaba yenu, na mimi ningeingia madarakani ningeanza kushirikiana na hao, na wengine walifikiria nitashirikiana nao, wamekwama mimi nitawatumbua kila siku ili Tanzania iwe ya neema iweze kwenda mbele, haiwezekani nchi kama hii tajiri, Tanzanite ipo, dhahabu ipo, wanyama mpaka nyani wameanza kuuzwa, wakimalizika nyani si tutauzwa na sisi ndugu zangu, ni lazima nisimamie hili" amesisitiza Dkt. Magufuli.

Aidha katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amewahakikishia kuwa serikali yake imeanza kuwashughulikia wafanyabiashara ambao wameficha sukari kwa makusudi na kusababisha upungufu wa bidhaa hiyo.

Rais Magufuli amesema tayari vyombo vya dola vimekamata tani 5,000 za sukari iliyofichwa na mfanyabiashara mmoja huko Tabata Jijini Dar es salaam na pia vimembaini mfanyabiashara mwingine aliyeficha sukari hiyo Jijini Arusha.

"Kweli nitawakomesha hawa, wasije wakanilaumu, haiwezekani ukaficha sukari wakati viwanda vyetu vinatengeneza sukari, kuna mmoja mwingine yupo Arusha hapa, nae ameficha sukari, alienda akanunua kwenye viwanda vya sukari vya hapa akaificha yote, leo ninamshughulikia.

"Kuna mwingine alinunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3,000 akaficha, na mwingine ameshikwa pale Tabata alikuwa ameficha tani 5,000, na wanasubiri katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ndugu zetu Waislamu wapate shida, haya ni mashetani makubwa, unawafichia watu chakula ambacho wanatakiwa kula, lakini nataka niwahakikishie ndugu zangu, hili ni tatizo la muda Tanzania, sukari itapatikana kwa wingi, na itanunuliwa na serikali, tumeshaagiza sukari lakini hatutawapa vibali hawa wafanyabiashara ambao wanatunyonya, tutanunua wenyewe na tutauza bei ya chini, hilo ndio lengo la serikali" Amesema Rais Magufuli

DONALD Trump Atashinda Uchaguzi USA..Akosekana wa Kumzuia


 
1.Wapinzani wa Donald Trump wamejitoa wote baada ya matumaini yao kumzuia kushindikana.
2.Hakuna namna tena ya kumzuia billionea Donald Trump kuwa mgombea urais wa Republican.
3.Chama cha Republican kinashuhudia mgawanyiko na mpasuko mkuwa kabisa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote.
3.Wanachama wa Republican wameonekana kuchoma moto kadi zao za uachama kama hasra zao kwa mgombea ambaye hawamtaki.
4.Wapo wanaosema hawatashiriki kabisa kupiga kura uchaguzi mkuu kwa kuwa Donald Trump hawamtaki na hawawezi kumpigia kura Hillary Clinton.Wapo ambao wanajiondoa katika chama.
5.Wapo wanaosema watalazimika kumchagua Hillary Clinton maana hawako tayari kuona Donald Trump anakuwa Rais wa Marekani.
6.Wapo wanaoona ni bora tu wakubaliane na hali na kumuunga mkono mtu ambaye hawamtaki kwa manufaa ya chama.
7.Aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W Bush mwenye umri wa miaka 91 amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hana mpango wa kumuunga mkono Donald Trump.
hii ni mara ya kwanza kwa George H.W Bush kutomuunga mkono mgombea wa chama chake cha Republican katika chaguzi zote.
8.Aliyekuwa rais wa 43 wa Marekani George W Bush(Junior ) naye amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hatamuunga mkono Donald Trump.
NB:Marais wastaafu wa Republican walio hai ni hawa Bush wawili kwa maana ya baba na mwana.
9.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2012 Mitty Romney amesema hatamuunga mkono Donald Trump na ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa hata kwenye mkutano mkuu wa kumtanganza mgombea pale Cleveland hatashiriki.
10.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2008 John McCain naye yupo mbioni kutoa taarifa rasmi.Taarifa za awali zinadokeza kuwa naye atachukua msimamo wa kutomuunga mkono Donald Trump na atajiweka kando katika uchaguzi huu.
11.Matajiri wapenzi wa chama nao wamegawanyika kama ilivyo hapo juu kwa makundi mengine wapo ambao wameonekana tayari kumuunga mkono Hillary Clinton kwa kuandika hadharani kauli mbiu ya Hillary Clinton I AM WITH HER (wakimaanisha wanamuunga mkono Hillary Clinton na si mgombea wa chama chao).
Joseph Mshinga.

BREAKING NEWS: KIMENUKA BUNGENI NDUGAI KUTOA TAMKO KALI KWA MWANASHERIA MKUU NA KUMTAKA APELEKE HARAKA SHERIA ITAKAYORUHUSU WATUMISHI WAZEMBE WAFUKUZWE KABISA KAZINI BADALA YA KUSIMAMISHWA KAZI NA KUSEMA HAYA.....

 

Spika wa bunge, Job Ndugai.
Dodoma. Spika Job Ndugai ametaka operesheni ya kushughulikia wazembe kazini iongezwe nguvu kwa kuunda sheria ya kuwatimua badala ya kuwasimamisha kazi kwa uchunguzi kama inavyofanyika sasa.
Ndugai, ambaye ni kiongozi wa Bunge ambalo kazi yake ni kutunga sheria, alimuomba Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumshauri Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupeleka haraka bungeni muswada wa sheria itakayoruhusu watumishi wazembe wafukuzwe badala ya kusimamishwa kazi.
Kauli ya Ndugai imekuja wakati Taifa likiwa kwenye mjadala kuhusu vitendo vinavyofanywa na viongozi wa Serikali vya kusimamisha watu kazi kwa kutangaza tuhuma zao kwenye mikutano ya hadhara na baadaye kuagiza uchunguzi ufanyike jambo ambalo wadau wa utawala bora na wanaharakati wanasema ni ukiukwaji wa sheria.
Wadau hao wanasema watuhumiwa hawana budi kuchunguzwa kwanza kabla ya kutangazwa hadharani kuwa wana makosa, wakisema kutofanya hivyo ni kushawishi uchunguzi ufanyike kwa lengo la kuwatia hatiani badala ya kutafuta ukweli.
Akizungumza kwenye kikao cha Makamu wa Rais na viongozi wa CCM mkoani Dodoma jana, Ndugai alisema sheria iliyotungwa ya watumishi wa umma si nzuri kwa kuwa inatumika kuwalinda hata wasiostahili kuwapo kazini kutokana na uzembe na ubadhirifu.
“Sheria za kuwalinda watumishi hazifai, ni bora mkamshauri AG azilete zote bungeni kwa wakati mmoja tuzipitishe ili wazembe na wabadhirifu wafukuzwe si kusimamishwa,” alisema Ndugai.
Alisema wakati mwingine amekuwa akishangaa kuona jinsi watu wanavyoharibu, lakini wakitaka kufukuzwa sheria inakuwa kikwazo na kulifanya Taifa kuingia katika hasara.
Alisema sheria hizo zikipelekwa bungeni atazisimamia zipitishwe haraka zote kwa wakati mmoja ili kuondokana na dharau inayofanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa na huruma na taifa lao.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa alikiri kuwa nafasi ya chama katika ngazi ya chini ni ndogo kwani CCM inaonekana kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa pekee.
Kimbisa aliwataka madiwani na watumishi wengine kutomwangusha Rais na badala yake waache kuwanyenyekea watumishi wa Serikali, bali wawawajibishe pale inapobidi.

PICHA 3: Hiki ndio kipigo cha Yanga kwa GD Esperanca ya Angola leo May 7 2016

 
May 7 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ambao mashabiki wao tayari mtaani wanajitamba na kujiita Mabingwa watarajiwa wa Ligi Kuu, walishuka uwanja waTaifa kuwakabili wapinazani wao GD Esperanca katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika.
IMG_0028
Yanga ambao walipangwa na GD Esperanca baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misrijumla ya goli 3-2 katika michuano ya klabu Bingwa barani Afrika, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wpinzania wao kutokea Angola klabu ya GD Esperanca, lakini Yanga watalazimika kwenda Angola wiki mbili zijazo kucheza mchezo wa marudiano.
IMG_0064
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa pande zote na kwenda mapumziko bila kufungana, lakini awali Eperanca walikuwa wanacheza mpira wa taratibu na kujitahidi kumiliki mpira ili kuituliza presha ya mchezo, hali ambayo ilifanya Yanga wabadilike na kufanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya 71 kupitia kwa Simon Msuva, kuingia kwaMatheo Anthony kulizaa matunda baada ya dakika ya 90 kufunga goli la pili.

Matatu ya kufahamu baada ya sukari tani 4,579.2 iliyofichwa kukamatwa Dar es salaam

 
May 06 2016 Rais Magufuli alizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Singida na Manyara wakati waliposimamisha msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kwenda Arusha. Rais Magufuli alitoa maagizo kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari kuanza kuisambaza mara moja, vinginevyo serikali itachukua hatua kali.
Sasa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa  kuwa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya suala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi. 
TAKUKURU ilitembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo, haya ndio waliyoyabaini…..
TAKUKURU imebaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo ili iweze kusambazwa
Katika eneo la Kitumbini kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.
Kumekuwepo na mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.

VIDEO: ‘Serikali isiruhusu wafanyabiashara waagize sukari nje’ Mbunge LijuaLikali

 
Baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwasilisha Bungeni Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2016/2017, Wabunge walipata nafasi ya kuchangia hotuba hiyo.
Hapa nakukutanisha na Mbunge wa Kilombero Lijua Likali ambaye yeye kaguswa zaidi na hii ishu ya uhaba wa sukari..>>’Leo ajabu karibu tani 8 za sukari zilikuwa kwenye godauni liliopo Tabata, hii tafsiri yake ni kwamba kuna sukari imefichwa na wafanyabiashara
Wakati Rais anania safi ya sisi kupata sukari na viwanda viendelee wao wanaficha sukari, kibaya baada ya upungufu hawa watu wanataka wapewe vibali vya kuagiza sukari.Hawa watu kwa tabia yao ni kwamba kwa hatuna hakika kama wataagiza ambacho wameruhusiwa
Mimi huwa najiuliza, hivi nia ya Serikali kubinafsisha hivi viwanda ilikuwa ni nini? ilikuwa ni kuwapa watu nafasi ya maeneo ya kufuga ama kuongeza uzalishaji na ajira?
Unaweza kuendelea kwa kumsikiliza Lijua Likali hapa chini kwenye hii Video…
ILIKUPITA HII BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI ZAIDI YA BILIONI 81 ILIVYOWASILISHWA BUNGENI?

Idadi ya Ajali zilizojitokeza wakati wa Majaribio Mabasi yaendayo Haraka


 
Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema kutozingatia sheria za barabara za mradi wa mabasi hayo, kwa vyombo vingine vya moto vimesabisha ajali 14 wakati madereva wa mabasi hayo wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya kuelekea kipindi cha mpito cha mradi kinachotarajia kuanza hivi karibuni.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Mhandisi Ronald Rwakatale amesema kuwa ajali hizo zimejitokeza wakati madereva wa mabasi ya mradi wakifanya mazoezi na kisha vyombo vingine vya moto viingilia barabara zake na kusabisha ajiali hizo.

Amesema ajali hizi ni matokea ya vyombo vingine vya usafiri kama magari madogo, daladala, bodaboda na waenda kwa miguu wamekuwa wakiingilia barabara za mabasi hayo na kusabisha ajali kutokana na kwamba barabara hizo haziruhusu mabasi hayo kupisha na vyombo vingine.

Mhandisi Rwakatale amesisitiza kuwa barabara za mabasi hayo ambazo ni za zege zimejengwa mahususi kwa ajili ya mabasi hayo hivyo madereva wa vyombo vingine wanahitajika kuheshimu sheria zinazoongoza mradi huo na kupita katika barabara walizotengewa na watakaokiuka sheria itachukua mkondo wake.

Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka unatarajiwa kuanza kipindi cha mpito mwezi huu wa Mei kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam

Rais Barack Obama Ataka Mienendo ya Muwania Urais wa Republican Donald Trump Ichunguzwe


UCHAGUZI MAREKANI: Rais Barack Obama ataka mienendo ya muwania Urais wa Republican Donald Trump ichunguzwe, asema urais sio maigizo.

Obama amesema matamshi ya mwanasiasa huyo yanafaa kuchukuliwa kwa uzito na kuwekwa kwenye mizani ili Wamarekani wapime iwapo anafaa kuwa Rais au hafai.

Obama amesema kauli za Trump haswa katika maswala ya usalama wa taifa na sera za kigeni ni za kutiliwa shaka na kusisitiza kuwa: "Urais hapa nchini sio mchezo wa kuigiza." Kadhalika Rais wa Marekani amevitaka vyombo vya habari kutoangazia tu kile alichokitaja kuwa kauli za kisanii za mwanasiasa huyo bali viangazie pia matamshi yake ambayo yanaweza kuzusha vita, kutia doa uhusiano wa Washington na nchi zingine na kuvuruga mfumo wa uchumi wa Marekani.

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Amtembelea Diamond Ofisini Kwake..Diamond Asema Haya

From @diamondplatnumz - Shukran sana sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam @PaulMakonda kwa kututembelea katika Office zetu za @Wcb_Wasafi jana usiku.... ujio wako Umetutia nguvu na Moyo mkubwa katika ufanisi wa kazi zetu.... Hakika wewe ni kiongozi wa pekee....Tunashkuru kwa Ushauri, muongozo wako mzuri na Muda wako wa thamani ulioupendekeza kwetu Jana!... ijapokuwa kaofisi ketu ndio kanaanza ila naamini uliona tunavyo hakikisha kudhibiti na kuzingatia USAFI Kuanzia Ofisini hadi Maeneo yatuzungukayo kama Mh Rais John Pombe na wewe Mlivyoagiza

KOCHA Jamhuri Kihwelo 'Julio' Ajigamba..Lazima Tuifunge Simba

 
Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema atahakikisha anashinda mchezo huo ili Yanga iwe bingwa.

Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Mwadui FC ni kesho Jumapili na inasubiriwa kwa hamu ile mbaya. Itapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 68 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 58, wakati Azam ina pointi 57. Yanga na Azam zimebakiwa na michezo mitatu, huku Simba wakiwa nayo minne.

Simba ikishinda mechi zake zote ikiwemo hii na Mwadui, itafikisha pointi 70, hivyo Yanga na Azam zikipoteza mechi zake zilizobaki, Wekundu wa Msimbazi wanaweza kuwa mabingwa.

Julio ambaye amewahi kucheza na kufundisha Simba, alisema hataleta urafiki kwenye mchezo huo na amepanga kushinda ili Yanga ipate ubingwa rasmi.
Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top