Loading...

YANGA Yashindwa Kutamba Kwa Waarabu..Yapokea Kichapo Bila Ubishi.....

Mabingwa wa soka la Tanzania bara Yanga SC wameanza vibaya kampeni zao za kuwania kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya MO Bejaia ukiwa ni chezo wa Kundi A.

Yassin Sahli alifunga bao pekee kwenye mchezo huo na kuipa pointi tatu MO Bejaia iliyokuwa ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani Stade de I’Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria.


Matokeo hayo yanaiacha Yanga katika nafasi ya tatu huku TP Mazembe wakiwa ndiyo vinara wa Kundi baada ya kushinda mchezo wao kwa magoli 3-0 dhidi ya Medeama ambayo inaburuza mkia.

Mazembe na MO Bejaia zinapointi sawa (pointi tatu) lakini TP Mazembe anaongoza kundi kwa tofauti ya magoli wakati Yanga na Medeama zikiwa hazina pointi lakini Yanga inakaa nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli. Medeama imefungwa magoli matatu wakati Yanga wameruhusu bao moja pekee.


Mchezo ujao wa Yanga utakuwa nyumbani (Dar es Salaam) June 28 itakapowaalika TP Mazembe kwenye uwanja wa taifa.

Breaking News: Maalim Seif Afunguka Kuhusu Lipumba, Amesema Alijiuzulu Mwenyewe Hakulazimishwa


Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif amejitokeza na kuongelea hatua ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. LIpumba ya kuomba kurudia nafasi ya Uenyekiti.

Amesema kwamba maamuzi ya CUF hufanywa kwenye vikao, tayari kuna kamati ya muda iliyoundwa na Baraza Kuu na hakuwezi kuwa na uongozi juu ya uongozi.

Amesema kuwa Lipumba alijiuzulu mwenyewe, bila kulazimishwa, alibembelezwa hadi na viongozi wa dini na akakataa na kuondoka.

Kuna Msanii Mkubwa Hakupenda Mimi Kujiunga na WCB – Rich Mavoko

Msanii mpya kutoka lebo ya WCB, Rich Mavoko amesema kuna msanii mkubwa bongo alimkataza kujiunga na WCB.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Rich Mavoko amesema kuna msanii mkubwa alimtumia ujumbe wa simu na kumuuliza kwanini amekubali kwenda kusimamiwa na Diamond.

Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz, kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujaje kwangu,” aliongeza.

Rich Mavoko amekuwa juu tangu alipojiunga na lebo hiyo ya WCB na kuachia wimbo wake ‘Ibaki Story’ unaozidi kufanya vizuri kwenye TV na Radio.

Yanga Imemuongezea Mkataba Mbuyu Twite, Lakini Imemtema Staa Wake Mmoja wa Kimataifa

Good news kwa mashabiki wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans, ikiwa imepita siku baada ya Yanga kufanikiwa kuwasajili wachezaji wawili golikipa Beno Kakolanya kutoka Tanzania Prisons na beki wa pembeni Vicent Andrew kutoka Mtibwa Sugar, leo June 7 wametangaza kumuongezea mkataba kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda Mbuyu Twite.

Yanga wamemuongezea mkataba wa miaka miwili Mbuyu Twite, lakini wamempa barua ya kuvunja mkataba kiungo wao wa kimataifa wa Niger Issafou Boubacar, hivyo huenda kukawa na mpango wa kumuongeza staa mwingine wa kimataifa atakayerithi nafasi ya Issafou Boubacar.

Uchaguzi Yanga kaa la moto

SARAKASI za nani ana haki ya kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Yanga, zimefungua taswira mpya kwa kuzikutanisha pande zinazosuguana pamoja na Serikali kujadili hatima uchaguzi huo
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imetangaza tarehe yake ya kufanya uchaguzi, huku ikisisitiza kutotambua mamlaka ya usimamizi wa uchaguzi wao kupitia Kamati ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambayo nayo imepanga tarehe yake.
Kikao hicho kitakachokutanisha pande tatu, TFF, Yanga na Baraza la Michezo la Tanzania (BMT) kitafanyika leo, Dar es Salaam.
Taarifa zilizopatikana jijini zilidai kuwa dhamira ya kikao hicho ni kutafuta suluhu ya kumaliza malumbano yanayoendelea kuhusu uchaguzi wa klabu hiyo ya Jangwani.
Katika kuonyesha uchaguzi huyo wa Yanga 'unaogopwa', mvutano huo ambao umekuwa gumzo kuanzia wiki iliyopita na kusababisha Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Aloyce Komba kujitoa, suala hilo halikujadiliwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana jana jijini.
"Kesho (leo) kutakuwa na kikao cha pande tatu, Kamati ya Utendaji halikujadili chochote," alisema mjumbe mmoja wa kamati hiyo iliyoko chini ya Rais Jamal Malinzi.
Naye kiongozi mwingine alisema walishangaa suala la Yanga kutokuwa sehemu ya ajenda zilizojadiliwa kwenye kikao hicho, wakati shirikisho limetajwa kukosa 'nguvu' katika uchaguzi huo kama ilivyokuwa kwa wanachama wengine.
"Uchaguzi wa Yanga haukujadiliwa na wala haukuonekana ni ajenda, na sisi wengine tunaona hatuna sababu ya kuuliza," alisema mjumbe mwingine (jina linahifadhiwa).
USAILI WAFANYIKA
Wagombea 19 waliopitishwa walipitishwa chini ya sekretarieti ya klabu walishiriki katika usajili kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uchaguzi utakaofanyika Jumapili Juni 11.
Orodha ya majina ya wagombea hao itatolewa leo na miongoni mwao ni Clement Sanga anayewania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, huku wanaowania nafasi nane za Kamati ya Utendaji ni pamoja na Samuel Lukumay, Salum Mkemi, Beda Tindwa, Lameck Nyambaya, David Ruhago na Ayoub Nyenzi.
Wengine ni George Manyama, Silvester Haule, Siza Lyimo, Hussein David, Hashim Mdhihiri, Athumani Kihamia, Pascal Laizer, Godfrey Ayoub, Bakari Malima, Mchafu Ahmed na Thobias Lingalangala.
Juni Mosi TFF ilisisitiza kuwa kamati yake ndiyo itasimamia uchaguzi wa Yanga Juni 25 na siyo Juni 11 kama Yanga wanavyotaka.

Tanzania Imetolewa na Misri Michuano ya AFCON 2017

June 4 2016 ilikuwa ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itacheza mchezo wake wa tatu wa Kundi G wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 AFCON, kwa kucheza na timu ya taifa ya Misri The Pharaos uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Huu ni mchezo ambao Taifa Stars alikuwa anahitaji ushindi wa aina yoyote ile.


Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa Taifa Stars, lakini ulikuwa ni mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Misri baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa Misri June 14 2015 katika mji wa Alexandria na kumalizika kwa Taifa Stars kufungwa jumla ya magoli 3-0, hivyo huu ulikuwa ni mchezo wa kulipa kisasi kwa Taifa Stars, lakini pia ulikuwa ni mchezo wa kutengeneza mazingira ya kufuzu AFCON 2017.


Hata hivyo timu ya Taifa ya Tanzania licha ya kuwa nyumbani imekubali kipigo cha goli 2-0, , magoli ya Misri yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea anayeichezea klabu ya AS Roma ya Italia Mohamed Salah dakika ya 43 na 58, kwa upande wa Tanzania Mbwana Samatta alikosa penati iliyopatikana baada ya Himid Mao kufanyiwa faulo ndani ya 18.

Kwa matokeo hayo Taifa Stars wanakuwa wametolewa rasmi katika michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017, lakini imebakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba itakayocheza September dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Misri imefikisha jumla ya point 10, Taifa Stars point moja na Nigeria ina point 2.

Hatuwaogopi Wamisri, Kesho Tutawafunga - Samatta

Samatta amesema, Misri ni timu ngumu na anaamini watakuwa wamejiandaa vizuri kwasababu wanajua mechi ya kesho ndiyo itawapa tiketi ya kuelekea fainali za mataifa ya Afrika mwakani lakini ni lazima watafugwa kwani Stars itakuwa inachezea Uwanja wa nyumbani.

Samatta amesema, hawaangalii kama wananafasi ya kupita au hawana nafasi lakini muhimu ni kuweza kupata ushindi wa aina yoyote haijalishi ni zaidi ya goli tatu au chini ya goli tatu wanachoangalia wao kama timu ni ushindi na kuweza kuwapa raha watanzania.

Samatta amesema, wachezaji wenzake wote wapo vizuri na kila mchezaji mawazo yake ni kuweza kufanya vizuri hapo kesho na wanategemea ushindi na sio sare wala kufungwa kwani watapambana kama timu ya Taifa na sio mchezaji mmoja mmoja.

Samatta amewataka watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa ili kuipa sapoti timu yao na watahakikisha wanawapa watanzania furaha kwa kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Amissi Tambwe Aishauri Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameushauri uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha unasajili kiungo mkabaji (namba sita), wa nguvu katika kipindi hiki cha usajili ambaye atakuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo.

Tambwe ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na mabao 21, amesema Yanga inakabiliwa na tatizo kubwa la kiungo mkabaji mwenye uwezo kupambana muda wote wa mchezo.

Alisema hali hiyo ndiyo imekuwa ikiisumbua timu hiyo katika mechi zake za kimataifa jambo ambalo uongozi wa timu hiyo unapaswa kulifanyia kazi katika kipindi hiki cha usajili.

“Tuna viungo wengi wazuri lakini bado tunahitaji kiungo mkabaji wa nguvu ambaye atakuwa anashirikiana vilivyo na mabeki wetu katika safu ya ulinzi.

“Uongozi wetu unatakiwa kuliona hilo na kulifanyia kazi katika kipindi hiki cha usajili kabla ya kuanza kushiriki michuano ya kimataifa ambayo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya timu tutakazokutana nazo,” alisema Tambwe.

Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu

wambura
Musa katika kinganyiro hicho aliwapiku Donald Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo Shooting. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Musa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga jumla mabao manne; mawili katika kila mechi.
Kwa kushinda tuzo hiyo ya Mei ambayo ni ya mwisho kwa msimu huu kwa wachezaji bora wa mwezi, Musa atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Washindi wengine wa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu wa 2015/2016 ambao mechi zake za mwisho zilichezwa Mei 22 mwaka huu ni Hamisi Kiiza wa Simba (Septemba), Elias Maguli wa Stand United (Oktoba), Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba), Shomari Kapombe wa Azam (Januari), Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari), Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi) na Juma Abdul wa Yanga (Aprili).

Manchester United yamfuta kazi Louis van Gaal

Image copyrightEPA
Image captionLouis Van Gaal
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United ,huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.Raia huyo wa Uholanzi anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya mitatu.Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi.Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United siku ya Jumanne.

BREAKING NEWS: DAR HAPATOSHI TENA BARABARA ZAFUNGWA NA MASHABIKI WA YANGA WAKIWA WANAWAPOKEA MABINGWA WA LIGI KUU>>>SHUHUDIA UMATI HUU HADI WANAKANYAGANA



Mabingwa wa Ligi Kuu, Yanga leo wameingia jijini Dsm wakitokea Angola na kupokewa na umati mkubwa wa mashabiki uliojitokeza na kuujaza Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Intenational Airport. Mashabiki hao hawakuishia Uwanja wa ndege, waliongozana na basi lililobeba wachezaji hadi makao makuu ya klabu hiyo Jangwani.
Neno moja tu la kuwakaribisha nyumbani wazee hawa wa 'KIMATAIFA'

HABARI NZITO: MBWANA SAMATTA AFANYA MAUAJI HAYA MAZITO KWENYE TIMU YAKE NA KUIPA USHINDI WA GOLI 5-2...SHUHUDIA BALAA LAKE HAPA

Mbwana Samatta amecheza dakika zote 90 za mchezo kati yake ya Genk dhidi ya Anderlecht na kuisaidia Genk kuibuka na ushindi wa magoli 5-2 katika kampeni za kuhakikisha timu yao inapata nafasi ya kushiriki michuano ya Europa League.

Anderlecht walianza kufunga goli la kuongoza dakika ya 25 kupitia kwa kiungo wao Filip Djuricic lakini goli hilo lilisawazishwa na Leon Bailey dakika ya 45 na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko timu zote zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1.

Kipindi cha pili Suarez aliiweka tena mbele Anderlecht kwa kuifungia bao la pili dakika ya 60 lakini dakika tano baadaye Buffel aliisawazishia Genk. Dakika ya 76, Pozuelo aliiweka mbele Genk kwa kutupia bao la tatu kisha Ndidi akaongeza bao la nne kabla ya Nikos Karelis hajamaliza shughuli kwa kufunga goli dakika ya 90 ya mchezo.

Samatta kucheza dakika zote 90 ni faraja kubwa kwasababu mchezo uliopita alitolewa kipindi cha kwanza wakati Genk ilipocheza na KV Oostende.

Samatta amesema sababu kubwa iliyopelekea kushindwa kuendelea na mchezo ule ilikuwa ni majereha aliyoyapata wakati wa kipindi cha kwanza cha mechi hiyo.

“Mechi iliyopit nilipata majeruhi kwenye kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, niliumia eneo la nyonga kwa hiyo baada ya kurudi vyumbani na kuwaeleza madaktari, waliniambia nipumzike kwasababu ningeweza kuendelea lakini wasiwasi ukawa ni kwamba huenda majeraha yangeongezeka halafu ingechukua muda zaidi kupona”.

“Kwahiyo madaktari waliamua nipumzike baada ya kupata maumivu, madaktari walijitahidi nipone haraka kwa ajili ya mchezo wa leo na jana nilifanya mazoezi pamoja na timu, kucheza au kutocheza kwenye mchezo wa leo ilikuwa ni mipango ya mwalimu.”

Endapo Genk watashinda mchezo wao wa mwisho siku ya Jumapili, watafuzu moja kwa moja kucheza Europa League lakini kama watamaliza wakiwa nafasi ya nne basi watalazimika kucheza play off nyingine dhidi ya mshindi wa play off II kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Europa.

TAARIFA MUHIMU: KOCHA MKUU WA TIMU YA TAIFA STARS "HARLES BONIFACE MKWASA" AMETANGAZA KIKOSI RASMI KITAKACHOMENYANA NA KENYA....HII NDIO ORODHA YA MAJINA YA WACHEZAJI

Taifa StarsImage copyrightTFF
Image captionTaifa Stars watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Harambee Stars 29 Mei
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi kitakachomenyana na Kenya Mei 29 uwanjani Kasarani, Nairobi.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote mbili kujiandaa kwa michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Bingwa Afrika mapema mwezi Juni, 2016.
TFF kwa kushirikiana na FKF zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 mwezi Juni.
Taifa Stars inatarajiwa kuingia kambini Mei 22, mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili Misri katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 4, mwaka huu.
Kikosi hicho kinajumuisha na:
Makipa: Deo Munishi ‘Dida’ (Yanga SC), Aishi Manula (Azam FC), Beno Kakolanya (Prisons FC).
Mabeki: Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam FC), Erasto Nyoni (Azam FC), David Mwantika (Azam FC), Juma Abdul (Yanga SC), Mwinyi Hajji Mngwali (Yanga SC) na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC).
Viungo: Himid Mao, Mohammed Ibrahim (Mtibwa Sugar), Shizza Kichuya (Mtibwa Sugar), Jonas Mkude (Simba SC), Ismail Issa Juma (JKT Ruvu), Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Farid Mussa (Azam FC), Juma Mahadhi na Hassan Kabunda (Mwadui FC).

BREAKING NEWS: YANGA YAFANYA MAUAJI MAZITO HUKO ANGOLA NA KUTINGA HATUA NYINGINE...HAYA HAPA MATOKEO YA MECHI YA YANGA NA ESPERANCE

YANGA YAPITA: Yanga yatinga hatua ya makundi CAF kwa jumla ya magoli 2-1 baada ya kufungwa 1-0 na Esperanca nchini Angola katika mechi iliyomalizika hivi punde.
Beki Nadir Haroub Canavaro ametolewa nje kwa 'red card' kutokana na rafu iliyozaa penalti ambayo imepanguliwa kishujaa na kipa Deo Munishi amepangua.

Ushauri kwa Mr Hashim Lundenga, Jitoe Miss Tanzania. Huaminiki tena

Nimeona kwenye habari hashim lundenga anaomba serikali imsaidie kutafuta wafadhili wa Miss Tanzania..

Kama yupo humu au jamaa yeyote aliyopo humu amfikishie huu ushauri.

Ni vizuri akakaa pembeni ya Miss Tanzania maana hakuna kampuni yeyote yenye akili itakayotoa pesa zake kwa Miss Tanzania ya lundenga...

Seke seke la Siti mtemvu ni kubwa sana limemvunjia sana trust... na kurudisha trust sio kazi ndogo.

Hata kama Lundenga anategemea shughuli za Miss Tanzania kupata hela yake ya kuishi... ni vizuri akatumia.mbinu za yeye kukaa pembeni na kuweka sura nyingine kama mwandaaji kwa ajili ya kupata trust ya mashabiki na wadhamini...

Ila yeye kama yeye mzee lundenga na skendo ya Siti Mtemvu hawezi fanikiwa tena kama enzi zile za zamani

Bomu feki laahirisha mechi ya Man United

Image copyrightPA
Image captionMashabiki waliokwenda kuangalia mechi wakishikwa na butwaa baada ya kuambiwa kuna bomu uwanjani Old Trafford.
Polisi nchini Uingereza imethibitisha kuwa kitu kilichokuwa kinadhaniwa kuwa ni bomu kilichoonekana kwenye uwanja wa timu ya Manchester United wa Old Trafford hakikuwa bomu kama ilivyodhaniwa bali kilikuwa ni kifaa cha wanausalama cha mazoezi kwa ajili milipuko.
Kifaa hicho kiliachwa na walinzi wa kampuni moja ya binafsi baada ya kufanya mazoezi yaliyowahusisha mbwa wenye kunusa vifaa na vitu vya kihalifu.
Kutokana na kuonekana kwa kifaa hicho mechi kati ya Manchester United na Bournemouth iliahirishwa.
Tayari kifaa hicho kimeshaharibiwa chini ya uangalizi mkali wa timu ya kuthibiti milipuko.
Tayari maafisa wa mji wametaka uchunguzi ufanyike na kuita kitendo hicho kuwa ni cha kizembe na cha kudhalilisha.
Maelfu ya mashabiki walioondolewa katika uwanja wa Old Trafford ambapo mechi baina ya wenyeji Machester United na Bournemouth iliahirishwa na itachezwa siku ya jumanne.

Riyama Afunguka Kutomsamehe Mtu Huyu kwa Kumdhulumu Pesa


 
MWIGIZAJI mahiri katika tasnia ya filamu Bongo Riyama Ali amelalamikia madalali wa kazi za wasanii kwa kuwa chanzo cha dhuluma kwa wasanii wanaotengeneza filamu, huku wao wakijinufaisha na jasho lao akiongaea na FC Riyama amedai kuwa ametapeliwa kazi yake ya Kajala.


hajui jinsi gani umepata fedha hadi kuunga unga na kutoa filamu bila ya huruma mtu anakudhulumu mimi kazi yangu Kajala hadi leo nimetapeliwa na mtu aliyeuza kwa Steps amenilipa pesa kidogo na filamu imetoka ina muda sasa,”

Msanii huyu amelalamikia mfanyabiashara maarufu kwa filamu za zaga zaga jina tunalihifadhi kuwa alichukua kazi yake kwa makubaliano kuwa anajuana na msambazaji haiwezi kukaa foleni hivyo angepata malipo yake kwa wakati lakini ameambulia kupewa fedha kidogo huku mtu huyo hapokei simu na kumtishia kuwa yeye anajulikana.

Aidha Riyama amedai kuwa Serikali na vyama vya wasanii viangalie jinsi ya kulinda maslahi ya wasanii wanaibiwa sana,kwani kumekuwa na tabia ya udalali wa filamu kwenda kwa wasambazaji ambao kazi ucheleweshaji ambao unajenga mazingira ya Rushwa.

“Nimekuwa na busara sana kwani nashangaa yeye kulipwa fedha huku filamu ikiwa kila kitu kimeandikwa mimi Riyama Ally ilikuwaje alipwe yeye bila mimi kuwepo?,”anasema Riyama Ally.

DONALD Trump Atashinda Uchaguzi USA..Akosekana wa Kumzuia


 
1.Wapinzani wa Donald Trump wamejitoa wote baada ya matumaini yao kumzuia kushindikana.
2.Hakuna namna tena ya kumzuia billionea Donald Trump kuwa mgombea urais wa Republican.
3.Chama cha Republican kinashuhudia mgawanyiko na mpasuko mkuwa kabisa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote.
3.Wanachama wa Republican wameonekana kuchoma moto kadi zao za uachama kama hasra zao kwa mgombea ambaye hawamtaki.
4.Wapo wanaosema hawatashiriki kabisa kupiga kura uchaguzi mkuu kwa kuwa Donald Trump hawamtaki na hawawezi kumpigia kura Hillary Clinton.Wapo ambao wanajiondoa katika chama.
5.Wapo wanaosema watalazimika kumchagua Hillary Clinton maana hawako tayari kuona Donald Trump anakuwa Rais wa Marekani.
6.Wapo wanaoona ni bora tu wakubaliane na hali na kumuunga mkono mtu ambaye hawamtaki kwa manufaa ya chama.
7.Aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W Bush mwenye umri wa miaka 91 amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hana mpango wa kumuunga mkono Donald Trump.
hii ni mara ya kwanza kwa George H.W Bush kutomuunga mkono mgombea wa chama chake cha Republican katika chaguzi zote.
8.Aliyekuwa rais wa 43 wa Marekani George W Bush(Junior ) naye amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hatamuunga mkono Donald Trump.
NB:Marais wastaafu wa Republican walio hai ni hawa Bush wawili kwa maana ya baba na mwana.
9.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2012 Mitty Romney amesema hatamuunga mkono Donald Trump na ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa hata kwenye mkutano mkuu wa kumtanganza mgombea pale Cleveland hatashiriki.
10.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2008 John McCain naye yupo mbioni kutoa taarifa rasmi.Taarifa za awali zinadokeza kuwa naye atachukua msimamo wa kutomuunga mkono Donald Trump na atajiweka kando katika uchaguzi huu.
11.Matajiri wapenzi wa chama nao wamegawanyika kama ilivyo hapo juu kwa makundi mengine wapo ambao wameonekana tayari kumuunga mkono Hillary Clinton kwa kuandika hadharani kauli mbiu ya Hillary Clinton I AM WITH HER (wakimaanisha wanamuunga mkono Hillary Clinton na si mgombea wa chama chao).
Joseph Mshinga.

Pesa Tulizowekeza Kwenye Muziki zimeanza Kurudi- Navy Kenzo

Kundi la muziki, Navy Kenzo ambalo linaundwa na wasanii wawili, Nahreal pamoja na Aika, ni moja kati ya makundi machache ya muziki nchini ambayo yanawekeza pesa nyingi katika kuandaa kazi zao.
Navykenzo

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Nahreal amesema tayari wameshaanza kurudisha pesa zao ambazo wamekuwa wakiwekeza kwenye muziki kwa muda mrefu.

“Gharama ambazo tumetumia ni kubwa na tunajua muziki ni uwekezaji, lazima uwekeze, kwa hiyo mwanzo tulikuwa tunaweka pesa nyingi lakini hazikuwa zinarudi, so tumefika wakati pesa imeanza kuingia. Kama tour yetu imetupatia pesa fulani, pia wimbo wetu ‘Kamatia Chini’ umetupatia deal kubwa. Kwa hiyo pesa ambayo tuliwekeza inarudi kwa njia nyingi, makampuni, show, na issue nyingine,” alisema Nahreal.

Pia katika hatua nyingine Nahreal amewataka mashabiki wake kusubiria kazi mpya pamoja na kolabo za kimataifa.

Bado Sijajua watu Wanaupendea nini Muziki wa Diamond Platnumz

Bongo ina wasanii wengi sana, kati yao 90% hawajui muziki kifupi ni wabovu akiwemo Diamond ila wanapendwa kupita maelezo, na 10% wanajua muziki kifupi ni wakali akiwemo Rama dee na Steve wa RnB ila cha kushangaza hawapendwi(muziki wao).

Sasa nashindwa kuelewa inakuwaje?? Mfano huyu Diamond miziki yake ni ya kawaida tu lakini raia wanamshobokea vibaya sana, kila ngoma anayotoa inakuwa ni national anthem lakini nikisikiliza mi naona ni miziki tu ya kawaida ambayo hata kwenye flash au laptop au memory card yangu siwezi kuweka.

Sijajua watu ni kwamba hawajui muziki au ni nini tatizo au ni ufreemason na uganga wa kupumbaza watu?? Kama ni mganga basi ni kiboko aisee, nasema ukweli ngoma za jamaa ninazozikubali ni Nitarejea na kesho, basi!
Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top