Loading...

Risasi Zarindima Zanzibar ........ Watu watatu Wajeruhiwa

Watu watatu wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na kupelekwa hospitali ya Alrahma kwa matibabu.

Majeruhi hao ni Yussuf Ali Juma (23), Ali Shaame Ibrahim (18) na Salim Masoud Bakar (18), wakazi wa Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja.

Kabla ya watu hao kujeruhiwa, milio ya risasi ilitawala jana majira ya saa 8:30 mchana katika mitaa ya Tomondo, Mwanakwerekwe na Kilimani, hivyo kuzua taharuki miongoni wakazi wa mitaa hiyo.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa waliyaona magari ya vikosi hivyo yakiendeshwa kwa mwendo kasi kuzunguka maeneo hayo huku yakiwa na askari wakifyatua risasi.

“Mimi kwa sasa nipo hapa Kilimani na hivi punde tu risasi tumezisikia kutokea upande huu wa Mwanakwerekwe na Jang’ombe na ghafla naona watu wanakimbizwa kuletwa hapa Alrahma” alisema Rashid Said (54), mkazi wa Migombani ambaye ni dereva teksi.

Majeruhi Ibrahim alisema: “Walikuja wale mazombi, wengine walifunika uso waliwafungua ng’ombe wetu na kutaka kuwachukua, kwanza wakapiga risasi juu, tulipoona wanawapakiza katika magari lao tukasogea ndipo wakatupiga risasi.”

Bakari Juma (35), mkazi wa Msheleshelini alisema: “Tunasikia hawa jamaa wanataka wauze kitoweo cha nyama siku za sikukuu peke yao, lakini miye nasema sawa wafanye hivyo, ila si kwa ng’ombe wa kupora.”

Baadhi ya wananchi walidai kuwa mifugo hiyo wakiwamo ng’ombe wa maziwa ni mali yao.

Mmoja wa wafugaji hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Omar alisema: “Sisi tunafuga ng’ombe hawa kama mnavyoyaona mabanda yetu yapo si miaka kumi wala ishirini ni tangu zamani wakati huo Tomondo ni pori tupu na mpaka sasa mifugo yetu haizururi wala haimkeri mtu yeyote.”

Licha ya askari kudaiwa kufika eneo la tukio na katika hospitali walikolazwa majeruhi hao, hali ya usalama ilionekana kuyumba pale makundi ya watu yalipohamasika kusogelea maeneo hayo.

Waliofika katika hospitali hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano kwa Umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Salim Abdalla Bimani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kufuatilia zaidi ili kubaini chanzo chake.

Hata hivyo, alisema polisi waliingilia kati na kwenda katika maeneo hayo kurejesha hali ya usalama.

“Sijapata kwa ukamilifu kilichotokea, lakini ni kweli hawa vikosi wanaendesha operesheni ya kukamata ng’ombe wanaozurura mitaani, wamekwenda huko na kukatokea kukwaruzana baada ya kuwepo vijana ambao hawataki kuondoa ng’ombe, nimepeleka askari kutuliza hali na sasa hali imekuwa ya amani”, alisema Kamanda Mkadam.

Mtoto wa Ajabu Mwenye Vichwa Viwili Azaliwa Geita


WANANCHI katika kijiji Kaseke kata ya Kasami wilayani na Mkoani Geita wamekubwa na taharuki na wasiwasi mkubwa mara baada ya  Geresi Saidi( 20) Kujifungua mtoto wa kiume mwenye vichwa viwili vinavyofanana sura.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jumapiri majira ya saa sita usiku katika katika kituo cha afya katoro alikwenda kujifungua muda mfupi baada ya kupata uchungu.

Channel Ten ilifika kijiji hapo na kushudia viumbe hao huku mamia yawananchi kutoka kila kona  wakifika na kushudia  tukio hilo na hapa mashuhuda wakaeleza ilivyokuwa.

Baba mzazi wa mtoto huo Stefano Lugisha amesema pamoja na mke wake kujifungua mtoto huyo lakini  ana imani kama ni mipango ya mungu kama amavyoeleza.

Diwani wa kata hiyo Anderea Karamura pamoja na mwenyekiti wa kijiji Zakaria Rukas wamewataka wananchi wao kutoliusisha tukio hilo na imani za kishilina swara hilo.

Akiongea kwa njia ya simu mganga kitua hicho aliyempokea mama huyona kumzalisha  Peter Janga amedhibitisha kutokea kwa na kwamba uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini nini tatizo kwa mama huyo ambaye hiyo ilikuwa ni nzao ya kwanza na kuongeza kuwa kiumbe hicho kilipoteza maisha baada ya muda mfupi.

Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp"

Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais kwenye mtandao wa WhatsApp.

Hapa cha muhimu ni kujuwa sheria hii inafanya kazi, inakamata, inahukumu na kufunga wananchi. Tutumie lugha ya staha, vijana hamko salama kwenye fb, twitter na WhatsApp...sheria ya mitandao ipo na inazunguka kama Simba aungurumae akitafuta mawindo

BREAKING NEWS: THE HOT NEWS NAPE NAUYE ATHREATINING DEATH OF SOME PEOPLE IN CCM AFTER DOING THIS THINGS.....


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema wakati wa mchakato wa chama kurejesha imani kwa wananchi hali ilikuwa ngumu kwake hadi kufikia kutishiwa maisha na watu wasiojulikana.

Mbali ya watu hao kumpigia simu za vitisho nyakati za usiku, pia walikuwa wakimchafua kupitia mitandao ya kijamii lakini anamshukuru Mwenyezi Mungu alivuka salama na chama kimevuka salama.

“Tulipoanza kuzunguka kujenga chama nilitukanwa sana. Watu waliwekeza kunichafua. Watu hao niliokuwa nawanyooshea kidole hawakufurahishwa na hatua ile hivyo wakaweka mkakati wa kutaka kunifukuzisha ndani ya chama na ilifika hatua wakawa wananichafua katika mitandao ya kijamii.

"Nikaamua kujitoa huko mpaka leo hii nimeamua kujitoa katika mitandao na kubaki katika twitter pekee kwa kuwa unaweza kutambua mtumiaji,” alisema Nape.

Akizungumza  nyumbani kwake mkoani Dodoma, Nape ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi na ambaye aliteuliwa kwa mara ya kwanza kushika nafasi hiyo mwaka 2011 Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alipounda sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu, William Mukama alisema watu hao walifikia kudai yeye si mtoto wa Mzee Moses Nnauye.

Kamati Kuu chini ya Mukama ilipita mikoani na kaulimbiu ya kuvua gamba iliyoasisiwa na chama kwa lengo la kuwaondoa watuhumiwa ufisadi lakini iliondolewa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2012 ikaundwa mpya chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.

Kukata vigogo
Katibu huyo wa uenezi alisema changamoto kubwa waliyokutana nayo katika mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM ilikuwa kukata majina ya waliokuwa viongozi wa Serikali ambao walijitokeza kugombea nafasi hiyo.

Nape alisema kumpata mgombea wa kupeperusha bendera ya chama hicho kongwe ilikuwa kazi nzito baada ya viongozi mbalimbali wa juu wa Serikali ya Awamu ya Nne kujitokeza wakiwamo, aliyekuwa Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhani.

Vigogo wengine waliowapa wakati mgumu CCM ni aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu na Nne, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, na mawaziri kadhaa lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu waliweza kutimiza wajibu wao.

“Kuwaondoa viongozi waliokuwa madarakani ni sawa na kutafuna jongoo kwa meno lakini hatukutetereka na hatimaye tukapata majina matano ambayo nayo yalipigiwa kura na kupatikana jina la mgombea mmoja,” alisema.

“Ingawa vikao vilikuwa vya moto sana na kulazimika kukesha mpaka usiku, kila mmoja alipata nafasi ya kujadiliwa na kutendewa haki siyo kama ilivyovumishwa kuwa wagombea wengine hawakujadiliwa,” alisema.

Nape alisema katika chama chao kila mwanachama ana nafasi sawa hivyo haikuwasumbua kuangalia majina ya watu hao wala nyadhifa zao badala yake waliangalia sifa za mgombea mwenyewe ndani ya chama.

Alisema anashukuru Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Jakaya Kikwete kwa kuwa na kifua cha kuhimili vishindo na hiyo ndiyo siri ya kufanikisha mchakato huo kwa kuwa ni mtoto wa CCM hivyo ilikuwa rahisi kumkata yeyote kwani uzoefu wake ndani ya chama ulisaidia.

Nape alisema itachukua muda mrefu kupata kiongozi kama yeye lakini pia hawawezi kupuuza kazi iliyofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana na wazee waliorekebisha mambo na kuvuka salama kwa kuwa hali ilikuwa mbaya.

Bunge laivu
Nape alisema suala la kuzuia kurushwa moja kwa moja kwa matangazo ya Bunge si lake na kwamba lilipitishwa na wabunge wenyewe.

“Mimi ni msimamizi wa Serikali. Watu wanapotosha, nilichofanya ni kulinusuru Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kwa miaka 10 mfululizo Bunge lilishindwa kuwalipa fedha zao ambazo ni Sh4.5 bilioni kila mwaka.

“Hili liwe fundisho kwa wabunge, kuna vitu wabunge wanapitisha hawavijui baada ya muda wanaona madhara yake wanaanza kulalamika kumbe walivipitisha wenyewe...Suala la Bunge kuanzisha kituo cha televisheni pia walilipitisha wenyewe, leo hii Katibu wa Bunge anavyotumia fedha kama ingekuwa haipo katika bajeti wasingemwacha,” alisema.

JESHI la Polisi Laendelea Kuikaba Chadema, Mahafali Mengine ya CHADEMA Yatawanywa

Jeshi la Polisi mkoa Kilimanjaro jana liliwatawanya wahitimu wa vyuo vikuu kupitia umoja wa Chadema (Chaso), waliokuwa wamekusanyika mjini Moshi kwa ajili ya mahafali yao.

Dalili za ‘kibano’ hicho zilianza kuonekana asubuhi wakati polisi na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa wamejihami kwa mabomu ya machozi, walipozingira hoteli ya Keys inayomilikiwa na Philemon Ndesamburo.

Hoteli hiyo iliyopo maeneo ya Kwa Alfonsi nje kidogo ya mji wa Moshi, ndipo ambako mahafali hayo ambayo yalikuwa yahusishe wahitimu 70 kutoka vyuo vikuu vinne yalikuwa yafanyike.

Wanafunzi hao ni kutoka Chuo Kikuu cha Mwenge (Mwekau), Chuo cha Kikuu cha Ushirika Moshi (Mocu), Chuo Kikuu cha Masoka na Chuo Kikuu cha Tiba KCMC (KCMU Co).

Hata hivyo, polisi wakiwa na magari yaliyokuwa yakipeperusha bendera nyekundu, walivamia hoteli hiyo na kuwataka wahitimu hao kutawanyika kwa amani, kwa vile mikusanyiko ya aina hiyo imezuiwa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) mkoani Kilimanjaro, Dickson Kibona alilaani tukio hilo akisema hakukuwa na sababu yoyote ya kuzuia mahafali hayo.

“Wamezuia bila sababu yoyote na hii inakiuka misingi ya kidemokrasia, Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa,” adai Kibona.

Kibona alidai kama isingekuwa kuhofia maslahi ya kibiashara ya Hoteli ya Keys ambapo kulikuwapo pia watalii, wangegoma kuondoka kwa kuwa hawakuvunja sheria yoyote ya nchi.

Mmiliki wa hoteli hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, alisema ndiye aliyewashauri vijana hao kutawanyika kwa amani na kuwataka wasibishane na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema polisi walipata taarifa kuwa wahitimu hao wangekuwa na mkutano wa kisiasa ambao ulijificha kwa mwavuli wa mahafali.

“Tumewaita viongozi wao na kuwaeleza kuwa mikutano yote ya kisiasa imezuiwa na watawanyike. Walituelewa na wakatawanyika, lakini sisi bado tunaendelea kuimarisha doria mitaani,” alisema.

Hili ni tukio la pili kwa wanachama wa Chaso kutawanywa na Polisi ambapo juzi katika hoteli ya African Dream mjini Dodoma, wahitimu wa vyuo vikuu mjini Dodoma nao walitawanywa na FFU.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema Chadema inaendelea kuhifadhi kumbukumbu za matukio yote yanayoendelea nchini, ili kujenga ushahidi utakaojitosheleza pindi itakapoonekana ni mwafaka kuchukua hatua zaidi.

Alifafanua kuwa chama hicho kinatambua hila zinazofanywa na Serikali kwa kulitumia Jeshi la Polisi, na kuwa wanatambua amri zinazotolewa na watendaji wa chama tawala kupitia wakuu wa mikoa na wilaya.

Alisema wanao ushahidi wa matukio yote utakaotumika muda wowote, watakapoamua kuishtaki Serikali ndani au nje ya nchi.

Ndoto ya Gwajima CCM kutimia

Dk. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM (Wakwanza), na John Magufuli, Rais wa TanzaniaNDOTO ya Josephat Gwajima, Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima inaelekea kutimizwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Hamis Mguta.
CCM kimeeleza kuwa, Dk. Jakaya Kikwete, mwenyekiti wa sasa wa chama hicho anatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa chama hicho kwa Dk. John Magufuli tarehe 23 Julai mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa leo na Christopher Ole Sendeka, msemaji wa CCM inaeleza kuwa, mkutano maalum utafanyika katika ofisi ndogo za chama hicho Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.
“Kamati Kuu imeridhishwa na maandalizi ya mkutano mkuu huo, Mkutano Mkuu maalum utatanguliwa na kikao cha sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa,” imeeleza taarifa hiyo.
Mei mwaka huu baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwepo kwa mgogoro ndani ya CCM kwamba, Dk. Kikwete kugoma kumkabidhi uenyekiti wa chama Dk. Magufuli, wiki iliyopita Mchungaji Gwajima aliibuka na kuishutumu CCM na mawakala wanaogomea Dk. Magufuli kukabidhiwa chama.
Mchungaji Gwajima aliishushia tuhuma CCM kwamba, lipo kundi la wanaCCM wanaozunguka sehemu mbalimbali nchini wakishawishi wanachama na wakimshawishi Dk. Kikwete ili aendelee na uenyekiti na kuleta hoja ya kutenganisha kofia ya Uenyekiti wa CCM na Urais wa nchi.
Kutokana na tuhuma hizo Ole Sendeka alisema, “napenda kuwafahamisha wana CCM, wapenzi wa CCM na wananchi kwa jumla kuwa, madai hayo ya Mchungaji Gwajima ni uongo mtupu na hayana hata chembe ya ukweli. Ni mambo ya uzushi na hadithi ya kufikirika.
“Watu hao hawapo kwani kama wangekuwepo habari hizo zingekwishajulikana chamani kupitia mfumo mahiri wa usalama na maadili wa ndani ya CCM.”
Muda mchache baada ya CCM kutoa taarifa hiyo, nyumba ya Mchungaji Gwajima iliyopo Mbezi Salasala ilizungumwa na polisi wakimsaka ambapo mkapa sasa inaripotiwa yupo nje ya nchi.
Tarehe 3 Mei mwaka huu Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa ya CCM ilikutana katika Ikulu ya Chamwino na kupitisha majina ya wagombea kwenye nafasi mbalimbali.
Kwenye mkutano huo Ole Sendeka alisema,“kimsingi kama ingekuwa ni kufuata Katiba ya CCM, Kikwete alitakiwa kukabidhi nafasi hiyo mwaka 2017 kwa malengo ya kutimiza kipindi cha miaka mitano lakini kutokana na utamaduni wetu, wameishakubaliana kukabidhiana majukumu hayo na sasa mandalizi yanafanyika.”

Breaking News: Jeshi la Polisi Lawatawanya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Dodoma Ambao ni Wafuasi wa Chadema Kwa Kufanya Mahafali Bila Kibali

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma  limewasambaratisha wanafunzi  wa vyuo vikuu  wanachama wa Chadema ( Chadema Students Organization -CHASO ) waliokuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika  Ukumbi wa African Dreams  ulipo Area D mjini Dodoma.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi wamekamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao.

Polisi wamesema mikusanyiko  yote ya kisiasa ilishapigwa marufuku, hivyo hata mahafali hiyo ilikuwa batili

Barua ya wazi kwa Freeman Mbowe na UKAWA wote

Na Thadei Ole Mushi.

Kama ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania mbinu ya wapinzania kutoka njee ya bunge kwa sababu mbali mbali haikuanza leo. Na tangu wameaanza kuitumia mbinu hii haijawahi kuwasaidia au hata kueleweka kwa wananchi badala yake sisi wananchi ndio huwa tunapata hasara.

Kwa mara ya Kwanza wapinzani walitoka njee ya Bunge wakati raisi Kikwete alipoingia madarakani kwa mara ya pili kwa kile walichokidai kuwa ni kutomtambua. Walitoka njee wakati wa kuhutubia bunge na kulifungua bunge.

Je waliposusia bunge mwisho wa siku hawakuja kumtambua raisi Kikwete?? jibu ni NDIO wakikuja kumtambua na walivunja rekodi kupiga hodi ikulu kuomba busara za raisi kuliko vipindi vingine vyote.Tuliwashuhudia wakiburudika na juice mara nyingi tu Ikulu wakipata picha ya pamoja nk.

Mara ya pili tunawaona upinzani ukitoka njee kususia bunge la katiba. Mwisho wa siku bunge liliendelea na katiba pendekezwa ikapitishwa bila kuwa na mawazo mbadala ya wapinzani ndani ya katiba ile inayosubiria kupigiwa kura.

Mara ya tatu upinzani unatoka njee kupinga matokeo ya uraisi yaliyompa raisi Magufuli ushindi. Wanatoka siku ya raisi kulifungua bunge kama walivyotoka kipindi cha Kikwete. Raisi analifungua bunge na baada ya hapo bunge lilelile lililopewa uhalali na rais Magufuli baada ya kulifungua wapinzani wanarudi na kulitumia. Na hata sasa wapinzani wameshamtambua raisi Magufuli kuwa ni raisi halali na aliyechaguliwa kihalali.

Mara ya nne ni hili la kumkimbia Dr Tulia. Katika hali ya kawaida nilifikiri wangelifanya hivi kwa siku moja tu. Mpango wa kususia kila siku kumetuathiri sana sisi wananchi kuliko kulivyomuathiri Dr Tulia. Tena wapinzani wanatoka njee kipindi muhimu kabisa ambacho walipaswa kuombea majimbo yao miradi ya kimaendeleo toka kwenye bajeti ambayo itapitishwa muda mfupi ujao.

Upinzani umetoka kwenye mstari wa kujenga hoja hadi kususia kususia mambo ya ajabu ajabu.Nakiri kabisa kuwa kilichoijenga kambi ya upinzani nchini ni hoja zao nzito miaka ya 2005-2015.

Sote tunakumbuka jinsi upinzani ulivyopata umaarufu kwa kujenga hoja za kukataa ufisadi, kudai katiba mpya, swala la Buzwagi, na hata juzi juzi swala la ESCROW. Kafulila pamoja na kutukanwa tumbili alisisimama kidete hadi akafanikiwa kuwangoa kina Warema bungeni na wengineo. Nataka nikuonyeshe nguvu ya hoja ilivyo na mantiki kuliko hii zomea zomea na kutoka nje ya bunge.

Katika nchi zote za jumuiya ya Madola Tanzania upinzani ndio unaongoza kwa kuthaminiwa kuliko nchi zote. Thamani hii upinzani umeshindwa kuutambua na kuutumia kujijenga badala yake wamekimbia na kinachowakimbiza ni kanuni walizojiwekea wenyewe.

Ni Tanzania tu katika ukanda huu Kambi rasmi ya upinzani inatambulika bungeni, kuwa na baraza la mawaziri kivuli, na baadhi ya kamati nyeti zinazogusa maslahi ya Taifa kuwekewa kanuni lazma ziongozwe na upinzani kama PAC nk.

Hii ni fursa ambayo upinzani walipaswa kuitumia kujitangaza kuliko kuzurura njee ya viwanja vya bunge. Inauma sana kuona wanakosea na hawataki kujirekebisha.

Naamini si wabunge wote wa upinzani wanataka kutoka njee ya Bunge lah hasha. Prof Elton Mayo aliwahi kutoa nadharia ya Hawthorne Effect, nadharia ya kisaikolojia ambapo mtu hufanya jambo kwa kuwa tu kuna mtu anayemsimamia kufanya hivyo au anafanya tu kwa kuwa anajua anaonekana anachokifanya. Hivyo unafanya jambo si kwa kuwa unapenda kulifanya ila unafanya kwa kuwa kuna sababu zinakufanya ufanye.Nikiangalia huu utoto anaoufanya Mbatia pamoja na uelewa wake wote naona madhara ya mob psychology.

MBOWE nakuomba usitumie tena mbinu hii haiwajengi inawabomoa.

Ole Mushi.

MwanaCCM mwenye kujali maslah mapana ya nchi.

BREAKING NEWS: TAARIFA MUHIM...CCM KIMENUKA SAKATA LA UWENYEKITI GIZA NENE HAKUNA KUKABIDHIANA KIJITI VIGOGO WAGOMA CHAMA CHATAJA WAGOMBEA HAWA AKIWEMO MWANDOSYA, MEMBE....

Katika kile kinachoonekana kama kuendana kinyume na desturi za chama,vigogo kadhaa wanajipanga kugombea Uenyekiti wa CCM Taifa. Taarifa za kiintelijensia za kichama zinawataja vigogo kama Prof. Mark Mwandosya,Jaji Agustino Ramadhani na Benard Membe kuwa kama wagombea watarajiwa wa Uenyekiti.

CCM,kwa miaka mingi iliyopita,imekuwa ikiacha kando matakwa ya kikatiba katika kumpata Mwenyekiti wa CCM Taifa. Kikatiba,Mwenyekiti anapaswa kuchaguliwa na wajumbe wa Mkutano mkuu wa Taifa wa CCM. Katiba ya CCM inatoa haki na nafasi kwa mwanachama yeyote wa chama chetu kugombea na kuchaguliwa.

Hatahivyo,tayari harakati za kichama zimeshaanza kumkabidhi Uenyekiti Rais John P. Magufuli. Huo utakuwa ni mwendelezo wa desturi kumpata Mwenyekiti kwa njia ya kukabidhiwa badala ya kuchaguliwa. Makundi mbalimbali chamani yanajipanga kusimamia Katiba ya chama kwa kugombea Uenyekiti. Umefika wakati wa kuheshimu Katiba ya CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza)

UKAWA Kususia Futari za Viongozi wakuu Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Dhihaka kwa Waislam

Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa wasiojua ni nguzo mojawapo kubwa katika Nguzo kuu za dini ya waislam. Na mwezi huu kwa waislam ni mwezi wa kufututrishana kusamehehana na kuombeana mema. Ata kama mnaugomvi mkubwa wengi huwa wanausubiri kwa ajili ya kusameheana ni mwezi wa rehema kwa waislam, Lakini kwa nchi yetu hatujafikia hatua mbaya ya kususia ata chakula au maji .

Ukawa wanachofanya ni kutaka kutengeneza Chuki baina ya watanzania ifikie hatua hatuzikani kisa siasa, Najiuliza tu km kiongozi wanayeshindana nae hakifiwa na mtu wa karibu yake Je wapo tayari kumsaidia au kumfariji??

Kama wameweza kususia Futari kisa yupo Naibu Spika?
Watanzania je tumefikia hapo

Uenyekiti wa Rais Magufuli CCM Waiva, Kamati Kuu ya Chama Hicho Kukutana Dar es Salaam Kesho

Maandalizi ya CCM kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti wa chama hicho ili ashike kofia zote mbili, yataanza kesho katika kikao cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

Taarifa kuhusu kikao hicho iliyotiwa saini na msemaji wa chama hicho, Christopher ole Sendeka ilisema: “Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM itafanya  kikao cha kawaida siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kitafanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete.”

Japokuwa taarifa hiyo haikueleza ajenda za kikao, habari kutoka ndani ya chama zinasema kikao hicho cha siku moja kinatarajiwa kujadili masuala mbalimbali, ukiwamo mchakato wa makabidhiano ya kiti hicho katika mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika mwezi ujao.

Kipindi cha uongozi wa chama kwa Kikwete kitamalizika mwakani, lakini imekuwapo desturi kwa rais mpya kuachiwa kofia hiyo mapema, hivyo Rais Magufuli anatarajiwa kurithi mikoba ya uenyekiti mwezi ujao.

Vilevile, kikao hicho kinatarajiwa kuhitimisha hoja zinazodaiwa kuibuka katika vikao vya ndani vya chama hicho kwamba CCM inataka kuvuruga utaratibu uliodumu kwa muda mrefu wa mwenyekiti kumwachia kijiti Rais aliyeko madarakani.

Madai kuhusu mkakati huo wa ndani yalisambazwa katika mitandao ya kijamii yakimnukuu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, lakini Ole Sendeka alisema hana sababu yoyote ya kumjibu kiongozi wa dini.

Februari 5, mwaka huu Kikwete alipokuwa anazungumza na wazee wa Manispaa ya Singida alisema sherehe za mwaka huu za maadhimisho ya miaka 39 tangu chama hicho kuanzishwa zilikuwa za mwisho kwake akiwa mwenyekiti, kauli ambayo iliashiria ataachia mapema uenyekiti.

Kwa desturi, wenyeviti wa CCM huwa wanaachia madaraka yao kabla ya muda wa uongozi wao kumalizika.

Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alikabidhiwa chama na Alhaji Ali Hassan Mwinyi mwaka 1996 badala ya 1997 na Mkapa alimkabidhi Kikwete kiti hicho mwaka 2006 badala ya 2007.

Kulingana na kalenda ya chama hicho, Mkutano Mkuu wa CCM kumchagua mwenyekiti unapaswa kufanyika mwaka 2017, lakini utafanyika mwaka huu kuendeleza utamaduni wa kung’atuka mapema.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa kinachoendelea sasa mikoani na wilayani ni maandalizi ya mkutano huo mkuu yanayosimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Bara, Rajabu Luhwavi kwa niaba ya Sekretarieti.

“Kikao hicho cha Kamati Kuu ndicho kitakachojadili ajenda za mkutano huo sambamba na kupanga tarehe ya kufanyika kwa mkutano mkuu,” zilieleza taarifa hizo.

Dk Magufuli anatajwa kuwa uongozi wake ndani ya CCM utakuwa wa kasi ya aina yake kutokana na hatua mbalimbali za ‘utumbuaji majipu’ anazozifanya ndani ya Serikali tangu Novemba 5, alipoapishwa kuwa Rais.

Wabunge UKAWA Wasusa Futari ya Waziri Mkuu

Wabunge wa vyama vinavyounda Ukawa jana walisusia futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ikiwa ni mwendelezo wa hatua za kususia shughuli zote zinazoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Riziki Ng’wale, alisema wamechukua hatua hiyo kutokana na Dk Tulia kuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo.

“Dk Tulia ndiye mgeni rasmi katika shughuli hiyo ya kufuturisha na sisi tumeamua kuwa hatutashiriki shughuli yoyote inayoongozwa naye,” alisema muda mfupi baada ya kutoka katika kikao cha wabunge wa kambi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alisema wamekubaliana wabunge wote wa kambi ya upinzani waliofunga watakwenda kufuturu majumbani kwao.

“Tumekubaliana hatutakwenda kufuturu bungeni na kila mbunge atakwenda kufuturu nyumbani kwake,” alisema.

Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha wapinzani kilichoketi chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia.

Futari hiyo ilitangazwa na Dk Tulia tangu juzi na kusisitizwa jana baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa mchana kuwa ingefanyika kwenye viwanja vya Bunge ambako wabunge wote walialikwa.

Kwa siku zaidi ya 10 sasa, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Dk Tulia kwa sababu hawana  imani naye.

Hali hiyo imefanya bajeti kuu kwa ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuchangiwa na wabunge wa CCM tu baada ya Dk Tulia kuongoza vikao kila siku, akiingia asubuhi na jioni.

Mwimbaji Ray C Katika Hali Mbaya Tena..Adhalilika Kinondoni Polisi Wamchukua..

Hali ya Kiafya ya Ray C imeleta Sinto fahamu baada ya Video inayozunguka mitandaoni ikionyesha akichukuliwa na Polisi huku akisema kuwa wanamteka....

Shuhuda wa tukio hilo ameandika haya hapa chini:

Esha Buheti
"Nashindwa hata niongee nini jamani, rayc Leo kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie rayc, I mean it jamani siku zote nlikua najua anaonewa ila nlichokishuhudia leoo nimeumiaa kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje? Nlikua na @kabulaflavour kino kwa wapemba tumefata chips mara tukaskia mtu anasema me rayc nataka kuvua nguoo, nikajua utani kushuka ni rayc anasema nishikenj kuna watu wanataka kuniteka, alikua na nguvu sana watu kamshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza kutafta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaaanza kugaragara kwenye matope akipiga KELELE kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari YA polisi ikambeba ila kwa tabu sanaa alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli mpk rayc anaondoka na ile gari yapolisi sikujua anapelekwa wapi alikua kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?"



BREAKING NEWS: ONE OF TANZANIA NEWSPAPERS REVEAL THE SECRET OF THE FORMER PRESIDENT MKAPA

IMG_20160617_050700

Breaking News: Polisi Waizingira Nyumba ya Askofu Gwajima


Taarifa zilizotufikia muda huu zinasema Polisi 6 wakiwa ndani ya Landcruiser wamezingira nyumbani kwa Askofu Josephat Gwajima.


Sababu za kufanya hivyo bado hazijafahamika, tutaendelea kuwajuza kadri tunavyoendelea kupata taarifa.

BREAKING NEWS: Taarifa ya CCM kukanusha Tuhuma Zilizotolewa na Askofu Gwajima


Bila ya shaka mmepata habari kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuwa siku ya Jumapili ya tarehe 11/06/2016 akiwa kanisani kwake, Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima alitoa kauli za uongo, uchochezi na uchonganishi dhidi ya Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli, Viongozi wa CCM, Watendaji wa CCM na Serikali ya Awamu ya nne.


Mchungaji Gwajima amedai ati kwamba lipo kundi la wanaCCM wanaozunguka sehemu mbalimbali za nchi wakishawishi wanachama na wakimshawishi Mwenyekiti wa sasa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ili aendelee na Uenyekiti na kuleta hoja ya kutenganisha kofia ya Uenyekiti wa CCM na Urais wa nchi.


Napenda kuwafahamisha wana CCM, wapenzi wa CCM na wananchi kwa jumla kuwa madai hayo ya Mchungaji Gwajima ni uongo mtupu na hayana hata chembe ya ukweli. Ni mambo ya uzushi na hadithi ya kufikirika.

Watu hao hawapo kwani kama wangekuwepo habari hizo zingekwishajulikana Chamani kupitia mfumo mahiri wa usalama na maadili wa ndani ya Chama cha Mapinduzi. Chama chenyewe kingekwishawatambua watu hao na kuwachukulia hatua zipasazo za udhibiti na nidhamu.


Kama mambo hayo yangekuwepo viongozi wa Chama wa Mikoa, Wilaya na Matawi waliofuatwa wangekuwa ndiyo wa kwanza kuwafichua.

Habari za namna hiyo hazijapokelewa kutoka popote na kutoka kwa kiongozi yeyote wa Chama. Kama kweli Mchungaji Gwajima anawajua watu hao awataje hadharani na aseme walikwenda kumuona nani, wapi na lini kufikisha ujumbe wao huo hasi dhidi ya CCM.


Napenda kusisitiza kuwa habari za namna hiyo hazipo katika Chama cha Mapinduzi. Kwa hakika kinachoendelea sasa Mikoani na Wilayani ni maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum ambapo Mwenyekiti wa CCM wa sasa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atastaafu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Joseph Magufuli atachaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya. Hakuna jambo lingine.


Nafurahi kuwafahamisha Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwamba kazi ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum inakwenda vizuri kabisa.

Shughuli hiyo inasimamiwa na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Rajabu Luhwavi kwa niaba ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Kwa mujibu wa hatua iliyofikiwa sasa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa inaweza kukutana siku yoyote kupanga tarehe ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kwa uhakika.


Sisi katika Chama cha Mapinduzi hatushangazwi ingawaje tunasikitishwa na kauli za uongo, uchochezi na uchonganishi za Mchungaji Gwajima dhidi ya Chama cha Mapinduzi.

Ana chuki iliyopitiliza dhidi ya CCM na Mwenyekiti wake. Yeye ni mtu ambae hajawahi kuitakia mema CCM. Hata yeye mwenyewe amekiri kwenye mahubiri yake ya tarehe 11 Juni, 2016 kuwa “alitaka CCM ishindwe katika chaguzi zilizopita na ndivyo anavyotaka iwe hivyo hata sasa, ili Chama chake cha upinzani kishinde.


Mchungaji Gwajima pia hana mapenzi na wala hamtakii mema Rais Dkt John Pombe Magufuli. Kwanza, hakutaka ashinde uchaguzi kwani alimpigania kwa hali na mali mgombea wa UKAWA. Pili, hataki adumu na kufanikiwa katika kazi yake ya Urais, ndiyo maana anatoa ushauri usiokuwa na mashiko na wakihasidi dhidi ya Mheshimiwa Rais.

Anamshauri ati kwamba atoke Chama cha Mapinduzi na kuanzisha Chama chake. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais lazima awe mwanachama wa Chama fulani cha siasa. Hivyo basi, Rais John Pombe Magufuli akitoka CCM anapoteza Urais na Makamu wa Rais anakuwa Rais na CCM inaendelea kuongoza. Yeye atakuwa hana chake.

Hivyo Rais wetu atakuwa amepata au atakuwa ameharibikiwa? Huo kweli ni ushauri wa mtu anayedai kuwa na mapenzi mema na Mheshimiwa John Magufuli? La hasha! Huo ni ushauri wa adui yake na wala siyo wa mtu rafiki na mwenye huruma na mapenzi na Rais wetu.


Mchungaji Gwajima anataka kufanya “danganya toto”. Napenda kumhakikishia yeye na genge lake kuwa “CCM hatudanganyiki na Rais Magufuli ndiyo kabisa “hadanganyiki na wala hababaiki”.

Mheshimiwa John Pombe Magufuli siyo kama Bwana fulani aliyekubali kudanganywa na Gwajima na kudanganyika. Alitoka CCM akiamini kuwa angeshinda. Aliyomtabiria hayakuwa na sasa yeye na wenzake wanajuta na wengi wameanza kukimbia.

Rais wetu mpendwa na Mwenyekiti wetu mtarajiwa hawezi kudanganyika kiurahisi namna hiyo. Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni mtu makini na mahiri.


Shabaha ya Mchungaji Gwajima ni kutaka kuleta mfarakano ndani ya Chama cha Mapinduzi kwa kumchonganisha Rais na Mwenyekiti wa CCM.

Anachotaka ni kukidhoofisha Chama cha Mapinduzi na kumdhoofisha Rais John Magufuli ili kupalilia Chama chake na mgombea wake washinde uchaguzi ujao.


Napenda kusema kwa kujiamini kuwa hilo halitatokea kamwe. Mwenyekiti Kikwete ni kada aliyelelewa na kupikika vyema na viongozi waasisi wa Chama na Taifa.

Anaelewa na kuheshimu mila na desturi nzuri ya CCM kuunganisha kofia ya Urais na Uenyekiti. Hawezi kwenda kinyume. Hakung’ang’ania Urais, hawezi kung’ang’ania Uenyekiti na wala hana mpango huo.


Hali kadhalika, hata ushauri wake wa kutaka Marais Wastaafu waondolewe kinga ili washitakiwe, shabaha yake ni ile ile ya kutaka kuleta mfarakano baina ya Rais John Pombe Magufuli na Marais wastaafu kwa lengo lile lile la kutaka kuleta mfarakano ndani ya CCM na nchini. Matumaini yake ni yale yale ya kudhoofisha CCM na Rais wake ili kunufaisha upinzani. Kamwe Rais wetu hatanasa katika mtego huo.


Kwa kweli inasikitisha kuona Kiongozi wa dini akitumia madhabahu takatifu kusema uongo na kupanga fitina na kupandikiza chuki katika jamii. Hatutegemei Kiongozi wa dini kuwa hivyo.

Hatukupenda kujibizana na Kiongozi wa dini lakini kwa vile ameacha ya dini na kuingilia ya upande wetu tumelazimika kusema. Wahenga wamesema “lisilobudi hutendwa”


Nawaomba wanaCCM na Wananchi kupuuza uongo, uzushi na ushauri hasi wa Mchungaji Josephat Gwajima.


Christopher Ole Sendeka.

Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi.

Mwili wa mvulana aliyenyakuliwa na mamba wapatikana

Maafisa wa polisi waliokuwa wakiutafuta mwili wa mvulana wa miaka 2 aliyenyakuliwa na mamba katika bustani ya shirika la Walt Disney World mjini Florida wameupata mwili wake.
Waogeleaji waliupata mwili huo ambao ulikuwa hauna majeraha yoyote na wanaamini ni ule wa mvulana huyo wa miaka miwili ambaye alinyakulwia na mamba na kuingizwa ndani ya maji siku ya Jumanne jioni mbele ya familia yake.
Mkuu wa kaunty ya Orange Jerry Demings amesema kuwa jina la mvulana aliyetoweka na mamba huyo ni Lane Graves kutoka Nebraska.
Tangu shambulio hilo mamba watano walikamatwa na kuuawa kwa lengo la kutafuta mabaki ya mwili wa kijana huyo.
Mwili uliopatikana majini bado haujatambuliwa rasmi lakini maafisa wa polisi wana imani ni ule wa Lane.
Mapema siku ya Jumatano maafisa wa polisi walisema kuwa hakuna tashwishi kwamba mvulana huyo alifariki.

Afrika Kusini yaadhimisha maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi

 
Afrika Kusini inaadhimisha miaka 40 tangu maandamano ya wanafunzi wa Soweto, walipopinga ubaguzi wa rangi katika elimu kwa kulazimishwa kusomeshwa kwa lugha ya Ki-Afrikaan.
Mamia ya wanafunzi walifariki katika vurugu zilizojiri wakati serikali ya ukoloni ya wazungu makaburu ilipotumia nguvu kupita kiasi, kujaribu kuzima maandamano hayo.
Maandamano hayo yalikuwa kama mwanzo wa kuelekea hatua za kumalizwa kwa utawala wa makaburu wa Afrika Kusini.
Makamu wa rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa, ameweka shada la maua kwenye kaburi la kijana Hector Pietersen


Ni picha ya mwili wa kijana huyo uliokuwa unabebwa na mwanafunzi mwenzake baada ya kupigwa risasi na polisi.
Picha hiyo ilibua hamasa na hasira kubwa na kuufanya ulimwengu kulaani ukatili uliokuwa ukiendelezwa na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo.

Picha/Video: Oscar Pistorius Atoa Miguu ya Bandia Mahakamani Kuonesha Udhaifu wake

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius Jumatano hii amelazimika kutoa miguu yake ya bandia ili kumuonesha jaji jinsi alivyo dhaifu na kwamba asingeweza kumuua mpenzi wake makusudi.
Kwenye kesi hiyo iliyokuwa ikioneshwa live kwenye TV, mwanariadha huyo alijaribu kutembea kwa tabu bila miguu hiyo.
T-shirt yake ilikuwa imeloa kwa jasho na macho kuwa mekundu kutokana na kulia.

Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top