MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila inatarajia kutoa hukumu Mei 17, mwaka huu.
Jaji wa mahakama hiyo anayesikiliza kesi hiyo mjini Kigoma, Ferdinand
Wambali, alisema kuwa amepanga kutoa hukumu tarehe hiyo baada ya pande
zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo yao.
Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Jaji Wambari aliomba kupatiwa muda
wa kutosha kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani
hapo ili aweze kutoa hukumu ya haki.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye
alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ni mshtakiwa wa tatu katika
kesi hiyo.
Katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila anaishawishi mahakama
itengue matokeo yaliyompa ushindi aliyekuwa mgombea wa CCM, Hasna
Mwilima badala yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa jimbo hilo.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Hasna,
aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye
alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria wa Serikali
ambaye anaiwakilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Katika kesi hiyo, Wakili Kenedy Fungamtama anamtetea Husna huku Kafulila
akitetewa na mawakili watatu, Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na
Daniel Rumenyela.
Post a Comment