Meya huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na kumsababishia maumivu makali.
Kesi hiyo jana ililetwa mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa ajili ya usikilizwaji ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja.
Wakili wa serikali Onolina Mushi alidai kwamba,kesi hiyo ililetwa kusikilizwa lakini mshitakiwa pamoja na wakili wake hawajafika mahakamani.
Kutokana na hali hiyo,aliiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na kupanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza shauri hilo.
Hakimu alikubali maombi hayo ikiwemo ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa Meya huyo.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji.
Katika kesi hiyo,Boniface anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 11, mwaka jana, maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam, kipindi hicho akiwa na cheo cha Udiwani kata ya Ubungo.
Ilidaiwa kwamba,mshitakiwa huyo alimpiga Lissa kwa mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali.
Shitaka la pili ilidaiwa kwamba ,mshitakiwa huyo katika tarehe hiyo kwa makusudi na kinyume cha sheria aliharibu kamera aina ya Nicon yenye thamani ya sh. milioni nane mali ya Kampuni ya Uhuru Publication Limited.
Post a Comment