Klabu ya Coasta Union ya jijini Tanga itahitaji miujiza pekee ili iweze kubaki katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao kutokana na hesabu kuonesha kuwa tayari timu hiyo imeshuka daraja.
Miujiza hiyo inatokana matokeo iliyopata leo katika dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga kwa kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji Stand United.
Mabao yote mawili ya Stand United katika mchezo wa leo yameupiwa wavuni na Elias Maguli katika dakika ya 29 kwa njia ya penati baada ya mchezaji wa Stand kuchezewa madhambi katika eneo la hatari, huku bao la pili akilipachika katika dakika ya 46, muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza, kabla ya Coastal kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa said.
Kwa mabao hayo sasa mshambuliaji Elias Maguli amefikisha magoli 14 na anakamata nafasi ya 4 katika orodha ya wafungaji wanaoongoza kwa mabao mengi zaidi akitanguliwa na Amis Tambwe (20), Hamis Kiiza (19), Donald Ngoma (16) huku akimuacha Kipre Tcheche na John Bocco wenye mabao 10 kila mmoja.
Matokeo haya yanaifanya Coastal kutangulia ligi daraja la kwanza huku ikiwasubiri wenzake wawili kutokana na kuwa na point ambazo haziwezi kuinasua kutoka katika nafasi tatu za chini hata kama itashinda mchezo wake wa mwisho uliobaki.
Kwa upande wa mechi nyingine zilizopigwa leo, JKT Ruvu imeibwaga Ndanda FC kwa mabao 2-0, huku
Mgambo JKT ikiilazimisha sare ya bao 1-1 Mtibwa Sugar
Hesabu zinaonesha kuwa baada ya michezo ya leo Jumamosi, Coastal Union imeendelea kubaki mkiani na point zake 22, ikiwa nyuma ya Mgambo JKT iliyofikisha pointi 24 ikiwa na mechi 2 mkononi, Kagera Suga yenye point 25 na mechi 3 mkononi, na African Sports ikiwa na point 26 na mechi 2 mkononi.
Kwa upande wake JKT Ruvu kwa kiasi kikubwa imejinasua kutoka katika dimbwi hilo la kushuka daraja baada ya ushindi wake wa leo ulioifanya ifikishe pointi 29.
Post a Comment