Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imekamilisha upelelezi wa
kesi ya rushwa inayowakabili wabunge watatu katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Wabunge
hao wa CCM ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali
za Mitaa (LAAC), ni Ahmed Saddiq (Mvomero), Kangi Lugola (Mwibara) na
Victor Mwambalaswa (Lupa).
Mwendesha
Mashtaka wa Takukuru, Godliver Kiriani aliiambia mahakama ya Hakimu
Mkazi, Thomas Simba kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliomba
ipangwe tarehe kwa ajili ya kuanza kuwasomea washtakiwa maelezo ya kesi
inayowakabili.
Hakimu Simba alipanga kesi hiyo ianze kusikilizwa Julai 4 baada ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Washtakiwa
hao ambao hadi jana hawakuwa na mawakili, wako nje kwa dhamana baada ya
kutimiza sharti la kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi
ya Sh5 milioni.
Wabunge
hao walipandishwa kizimbani na Takukuru kwa mara ya kwanza Machi 31,
2016 na kusomewa mashtaka na wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kwa nafasi zao za ujumbe wa LAAC, waliomba rushwa ya Sh30
milioni kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Gairo, mkoani Morogoro, Mbwana Magote ili waweze kutoa mapendekezo
mazuri ya Taarifa ya Hesabu za halmashauri hiyo za mwaka 2015/2016.
Wanadaiwa
kutenda kosa hilo, Machi 15, 2016, kinyume cha kifungu cha 15 (2) cha
Sheria ya Takukuru, wakiwa katika Hotel ya Golden Tulip, iliyoko eneo la
Masaki, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Post a Comment