Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Ben Pol amesema hatua ya Diamond kuamua kumsaini Rich Mavoko katika label ya WCB, itafungua njia kwa wasanii wengine kuwa na moyo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.
“Ni vizuri sisi kwa sisi tukaaminiana na kufanya kolabo kwenye kazi,” alisema Ben Pol. “Diamond ni mpiganaji na Mavoko ni mtu ambaye ana kipaji na mjanja mjanja, kwa hiyo muungano wao unaweza kuleta mapinduzi makubwa katika muziki,”
Pia muimbaji huyo amewataka wale wasanii wenye uwezo wa kuwasaidia wenzao wasisite, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuupeleka muziki wa Tanzania mbele zaidi.
Post a Comment