JENERALI ULIMWENGU AMRUSHIA KOMBORA JK
Mwanaharakati Jenerali Ulimwengu amesema Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete anapaswa kushtakiwa kama viongozi wengine walioisababishia hasara Serikali.
Akizungumza katika tamasha la Nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ulimwengu amesema fedha nyingi zimepotea wakati wa kuunda Katiba Mpya ambayo haikupatikana.
Hata hivyo, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo, amesema badala ya kumlaumu mtu mmoja mmoja, mjadala mpana wa kitaifa unahitajika kujua kilichosababisha Taifa kukosa Katiba Mpya.
“Hakuna anayeandika ni wapi tulipokwama, tunalaumu na kumjadili mtu. Wengine wanasema katiba imekwamishwa na watu wachache…tunapaswa kuwa na mjadala wa kina kujua ni wapi tulipokwama,” amesema Mkapa.Akiwasilisha mada, Mkapa amesema si kwamba Mwalimu Nyerere hakupenda kampuni binafsi zije kuwekeza nchini bali alipenda biashara na uwekezaji ufanyike kwa haki, usawa na kuchangia maendeleo ya nchi
Post a Comment