Rais wa Marekani
Barack Obama ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea
urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye
mwaka huu nchini Marekani.
Amechukua hatua hiyo muda mfupi baada
ya kukutana na seneta wa Vermont Bernie Sanders ambaye amekuwa
akikabiliana na Bi Clinton katika kinyang’anyiro cha kumchagua mgombea
wa chama hicho.Akizungumza kwenye video ambayo imepakiwa kwenye Twitter na Bi Clinton, Bw Obama amesema mgombea huyo ndiye aliyewahi kuhitimu zaidi kuwa rais wa Marekani.
“Niko pamoja naye, nina msisimko na nasubiri sana kutoka huko nje na kufanya kampeni na Hillary,” amesema Obama.
Wawili hao sasa wanatarajiwa kuanza kufanya kampeni pamoja.
Bw Sanders naye amesema yuko tayari kufanya kazi na mpinzani wake, Bi Clinton, kumshinda mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi mkuu.
Hata hivyo hakujiondoa kinyang’anyironi. Alisema ataendelea kufanya kampeni yake na kwamba anatumai atakutana na Bi Clinton hivi karibuni.
Post a Comment