Wanajeshi tisa wa Muungano wa Afrika
wameuawa na wengine sita kujeruhiwa wakati wa shambulizi lililoendeshwa
na wanamgambo wa kiislamu wa al-Shabab katika moja ya kambi zake.
Waziri
wa ulinzi nchini Somalia Abdirisak Omar Mohamed, alikiambia kituo cha
radio cha serikaili kuwa, wanamgambo 240 waliuawa wakati wa shambulizi
hilo.Kwa upande wake al-Shabab wanasema kuwa wamewaua wanajeshi 60 wakati wa shambulia hilo, huku AMISOM ikiwa haijasema ikiwa wanajeshi wake waliuawa.
Wenyeji wa eneo hilo waliiambia BBC kuwa walisikia mlipuko mkubwa uliofuatiwa na ufyatulianaji mkali wa risasi.
Post a Comment