Msemaji wa Kambi ya Upinzani, David Silinde amesema uamuzi wa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kuwa wabunge wanaomsusia wasilipwe posho kwa sababu wamekuwa wakisaini na kutoka nje, hauwatishi na wataendelea kufanya hivyo.
“Mbunge akisaini analipwa posho hiyo iko kwa mujibu wa kanuni, sasa yeye Dk Tulia juzi alipotoa mwongozo alianza na kanuni lakini baadaye akaingia kwenye taratibu tofauti, kwamba mbunge akisaini na kutoka hatalipwa, hapo amechemsha,” alisema Silinde.
Alisisitiza kuwa hatua hiyo ni kinyume na utaratibu, kwani kiongozi huyo wa Bunge alitoa hukumu ya kesi inayomhusu yeye mwenyewe.
Post a Comment