Serikali ya
Tanzania imesema zaidi ya wasichana 500 raia wa nchi hiyo wanatumikishwa
katika kazi hatari zikiwemo za ukahaba katika nchi za Asia na Uarabuni.
Taarifa
ya wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imesema imepata taarifa kuwa kuna
mtandao unaowasafirisha wasichana katika nchi hizo kwa madai ya kufanya
kazi za ndani lakini baadae hutumikishwa kwenye biashara ya ngono.Taarifa zinasema baadhi ya wasichana hao wemekimbilia kwenye ubalozi wa nchi hiyo ili kuomba kurudishwa nyumbani
Mindi Kasiga ni Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ambaye anasema ''
Mtandao huo unachofanya ni pamoja na kuwatafuta wasichana wenye umri kati ya miaka 18 na 24 na hata chini ya umri huo na kuwalaghai kuwa kuna fursa za ajira katika mahoteli, migahawa, maduka makubwa au kazi za nyumbani nchi za nje na kwamba watawasaidia wasichana hao kupata kazi hizo pamoja na kuwawezesha kupata vyeti vya kusafiria VISA na tiketi za ndege kwa ajili ya kusafiri kwenda kwenye nchi husika''.
Wengi wa watu wanaokumbana na ahadi hizo, wanavutika kirahisi kwani wanaona hiyo ni fursa ya kujipatia ajira na kipato cha uhakika.
Kwa taarifa tulizozipata kuhusiana na mtandao huo ni kwamba wengi wa Watanzania wanoenda India,
Hulazimishwa kufanya ukahaba na kunyang'anywa hati za kusafiria ili kuwadhibiti wasitoroke, ndiyo matatizo makubwa zaidi ambayo yamekuwa yakiwakabili Watanzania.
Kufuatia matumaini wanayojengewa na walaghai vijana wa Kitanzania wamejikuta au wamelazimika kukubali kufanya kazi za ukahaba ili kurejesha gharama za kuwasafirisha kutoka Tanzania kwenda katika mataifa hayo ili waweze kurejeshewa
Hati zao za kusafiria pamoja na kupata nauli kwa ajili ya kurudi Tanzania.
Baada ya kuona changamoto hizi zinazowakumba Watanzania wanaokwenda kufanya kazi za ndani nchi za Mashariki ya Kati.
Balozi za Tanzania katika ukanda huo ziliaandaa utaratibu maalumu kwa wafanyakazi wanaokwenda kufanya kazi katika nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuandaa mikataba kulingana na sheria za nchi husika.
Kwa upande wa Mashariki ya Kati, kuanzia Juni, 2015, Serikali iliamua kukataza rasmi Watanzania kwenda kufanya kazi zisizo na ujuzi au za ndani katika nchi hizo hadi utaratibu maalum wa kisheria utakapoandaliwa.
Baada ya marufuku hiyo , Wizara ikishirikiana na wadau husika iliitisha vikao ili kujadili namna nzuri ya kupata suluhisho la kudumu kuhusu changamoto zinazosababishwa na mtandao huo.
Huku bi lilian Liundi,Mkurugenzi wa mtandao wa jinsia Tanzania anaona tatizo lipo kwenye nchi zetu za kiafrika bado azijatengeneza mifumo mizuri ya ajira na elimu,kwani ndio chanzo cha wasichana au vijana kurubuniwa kiurahisi kwenda nje kutafuta ajira na mwisho wa siku wanaishia kudhalilishwa.
Post a Comment