Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umesema Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala.
Sumaye ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri mkuu lakini hakufikia hata theluthi ya utendaji unaofanyika sasa.
Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata mbili za kwandele na mbichi jimbo la Rombo mkoani kilimanjaro.
Shaka alisema anachokifanya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi wameyasahau.
Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita Sumaye.
Aidha Kaimu huyo alimuonya Sumaye kuacha kumfuatafuata Dk Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazozichukua dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini.
Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima kina sumaye na wenzake wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa.
Pia shaka aliwataka wananchi wa jimbo la Rombo kujitayarisha ili kumpiga chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwa sabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
"Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, Selasimi hajui anachokifanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisitiza shaka
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagombea wa nafasi mbali mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba.
Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi ya asili au ujamaa.
"Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, hakutuacha tukiwa tumegawanyika , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni kwasabahu hilo ni balaa au janga katika jamii "alisema Raib.
Jumla ya wanachama wapya 103 walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na mahare wilaya ya Rombo.
Post a Comment