Loading...

BREAKING NEWS: MAWAKILI WANAO IHUJUMU SERIKALI YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI WAKIONA CHAMOTO....


WIKI moja baada ya Serikali kutangaza kuanzishwa kwa Divisheni ya Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu, Rais John Magufuli amewaibukia mawakili wa Serikali, akiwatuhumu kwa kushirikiana na mawakili wa wahalifu ili Serikali ishindwe kesi. Aidha amewaonya polisi kwa kuingia mikataba inayotia mashaka baina yao na wawekezaji.Mahakama ya ufisadi inatarajiwa kutumika kushughulikia watuhumiwa wa rushwa na ufisadi, wakiwemo waliokwisha tumbuliwa, lakini kesi zake zinatarajiwa kuanza kunguruma Julai mwaka huu.

Akizungumza mkoani Dodoma jana wakati akifungua kikao kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa Serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi, Rais Magufuli alisema mawakili hao wakiona kesi inayohusu fedha imeingia, wanasema ‘dili’ limeingia.

“Kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache, nasema wachache… Panapokuwa na kesi inayohusu fedha, wana misemo yao wanasema dili limepatikana.

“Saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wanashirikiana na mawakili wa Serikali na mawakili wanaomtetea mhalifu na wanaposhirikiana siku zote Serikali inashindwa,” alisema.

Alionya kuwa hali hiyo inapoonekana kila siku Serikali inashindwa katika kesi, kunakuwa na kigugumizi cha kuwezesha mawakili hao pale wanapopeleka maombi.

“Niwaombe mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslahi ya nchi mbele,” alisema na kuongeza kuwa amekuwa akisikitishwa na vitendo vya Serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top