Loading...

Akaunti ya Instagram ya Linah yenye Followers milioni 1.3 Yadukuliwa (hacked)

Akaunti ya Instagram ya Linah yenye followers milioni 1.3 imedukuliwa (hacked) Jumanne hii.

Tayari hacker huyo ameibadilisha jina akaunti yake na kuipa jina ‘suponzetrie’ huku akifuta picha zake zote alizoziweka mwaka huu.

Post ya mwisho inayoonekana sasa ni video ya tamthilia ya Empire aliyoiweka December 27, 2015. Haijulikani nini lengo la hacker huyo na kama ni wa hapa hapa Tanzania.

Linah anakuwa msanii wa hivi karibuni ambaye akaunti yake ya Instagram imedukuliwa. Miezi kadhaa iliyopita akaunti ya Shilole pia ilidukuliwa japo alifanikiwa kuirejesha.

“Jamani daaaah ndo kama hivyo watu washafanya yao pole kwa uwezo wa Allah itarudi,” Shishi amempa pole Linah.

Zaidi ya kujitangaza, miaka ya hivi karibuni akaunti za mastaa zimekuwa moja ya vyanzo vyao muhimu vya kipato na wale wenye followers wengi wamekuwa wakipata deals zenye hela nyingi.

Ni wazi Linah atakuwa kwenye wakati mgumu kwa sasa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top