Loading...

Serikali yaumbuka–Bajeti hewa

 John Magufuli, Rais wa Tanzania
SERIKALI ya Dk John Magufuli imeumbuliwa na kambi ya upinzani, imeumbuka kwa kupeleka bajeti hewa itakayopitishwa na wabunge wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Josephat Isango. 
David Silinde, Waziri Kivuli Wizara ya fedha na mipango amebainisha hayo bungeni na kueleza kuwa mfumo wa bajeti wa mwaka 2016/17’ unaonyesha kuwa kiasi cha shilingi trilioni 7.475 hazipo na pia hazionekani zitakopwa kutoka benki gani na kasma yake haionekanai katika vitabu ambavyo bunge litapitisha.
Akisoma hotuba yake huku akinukuu ibara ya 137(1) Silinde amesema  mwaka huu wa fedha 2016/17 serikali imewasilisha bajeti hewa Bungeni.
Mheshimiwa Spika, ninasema kuwa serikali hii imeleta bajeti hewa hapa Bungeni na nitathibitisha maoni yangu haya kama ifuatavyo;
Kwa mujibu wa kitabu cha mapato ya serikali katika mwaka huu wa fedha kilicholetwa hapa bungeni kinaonyesha kuwa mapato yote ya serikali yaani mapato ya kodi, yasiyokuwa ya kodi ,mikopo na misaada ya kibajeti itakuwa jumla ya shilingi Trilioni 22.063.” alisema Silinde.
Alifafanua kwamba upatikananji wa mapato yatokanayo na kodi na tozo mbalimbali ni shilingi Trilioni 17.797 mapato yasiyokuwa ya kodi ni shilingi Bilioni 665.664 huku misaada ya kibajeti ikiwa ni shilingi Trilioni 3.600Silinde alishauri kuwa ni muhimu wabunge wakatambua kwamba Serikali hii haijaonyesha chanzo kingine kipya cha mapato ambacho hakijathibitishwa na au kupitishwa na bunge hili kwa mujibu wa katiba na ijulikane pia kuwa bunge halipitishi kitabu cha hotuba ya waziri bali hupitisha mafungu yaliyopo kwenye vitabu vya bajeti ya serikali.
Aliongeza kwamba kwa mujibu wa kitabu cha matumizi ya kawaida na kitabu cha Maendeleo, kama vilivyowasilishwa bungeni, tayari bunge limeshaidhinisha matumizi ya jumla ya shilingi Trilioni 23.847 Alibainisha kuwa mchanganuo wa fedha halali ambao bunge litapitisha ni shilingi 13,336,042,030,510 fedha za matumizi ya kawaida  pamoja na Shilingi 10,511,945,288,575  fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Kutokana na takwimu hizo Silinde alibainisha kuwa kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/17 iliyowasilishwa kwenye mkutano wa wabunge wote katika ukumbi wa Julius Nyerere 06 Aprili, 2016 pamoja na maelezo ya hotuba yake aliyoyatoa hapa bungeni uk. 91 Dk Philip Mpango ameendelea kulidanganya bunge na dunia kuwa katika mwaka huu wa fedha serikali ina bajeti ya kiasi cha shilingi Trilioni 29.539.
Juhudi za kumpata Dk Mpango kwa ufafanuzi bado zinaendelea.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top