Mkutano wa tatu, kikao cha sita umeendelea tena leo April 28 2016 bungeni Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kayajibu baadhi ya maswali kutoka kwa Wabunge, moja ya swali kutoka kwa Mbunge wa viti maalum CHADEMA Kunti Yusuph Majala lilikuwa>>
‘Kwanini Serikali imekuwa ikipitisha mikataba bila kupita bila kushirikisha Bunge?‘
Majibu ya Waziri Mkuu Majaliwa yakawa>>>’Ni kweli Bunge linafanya kazi ya kuisimamia Serikali, lakini yapo maeneo ambayo Bunge lenyewe limetoa mamlaka ya kwa Serikali kuendesha shughuli zake ikiwemo kupitisha mikataba‘
‘Utaratibu ambao umewekwa kikatiba, tumemtumia Mwanasheria mkuu wa Serikali, Mwanasheria mkuu ni miongoni mwa watu wanaotambulika katika katiba ya Tanzania‘ –Waziri Mkuu Majaliwa
Baada ya Majibu ya Waziri Mkuu Mbunge Kunti hakuridhika na majibu na yakatokea haya mengine kwenye hii video
Post a Comment