Loading...

BREAKING NEWS: WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI MH: NCHEMBA AVUNJA RIKODI YA MWAKA HUKO BUTIAMA, SIKILIZA KAULI ALIZOTOA ZA KUMKAMATA AFISA ARIDHI WA WILAYA YA BUTIAMA

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba aagiza afisa ardhi wa wilaya ya Butiama ndg.Clavery Bitabile akamatwe mara moja na vyombo vya dola vichukue hatua kwa kosa la kuuza eneo la mnada wa upili(Mnada wa Mifugo) wa Kirumi uliopo wilaya ya Butiama.

Mbali na kuuza eneo hilo na kutoa hati kwa mtu binafsi wakati tayari eneo hilo la serikali la mnada lilikuwa na hati,Bwana Bitabile amekuwa kinara wa kusababisha migogoro kadha wa kadha katika wilaya ya Butiama na jimbo la msoma vijijini kwa muda mrefu.Moja ya migogoro mikubwa anayotajwa kusababisha ni ule wa shamba la Buhemba(Mikamariro) n.k

Mwigulu Nchemba akitoa agizo hilo,amesisitiza pia vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa haraka ili mnada huo uanze kufanya kazi. Hatua hii ni mwendelezo wa ziara ya Mh.Mwigulu nchemba kukagua maeno mbalimbali yanayohusiana na wizara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Jioni ya leo,Mwigulu atakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara Tarime mjini kuzungumza na wananchi kuhusu dira ya wizara yake katika kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa pembejeo,ufugaji wa kisasa na uvuvi salama.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top