Loading...

‘KUPATA TAARIFA NI HAKI YAKO YA MSINGI, IDAI’

 

Mnamo Machi 18 mwaka huu iliripotiwa tukio la utekaji nyara kwa Mwandishi wa Kituo cha Deutsche welle (DW) na Gazeti la Mwananchi, Salma Said kwa kile kilichodaiwa kuwa jinsi alivyokuwa akiripoti habari za Uchaguzi wa Marudio Visiwani Zanzibar.

Mei 3 kila mwaka Dunia huadhimisha  Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD), ambapo hapa nchini maadhimisho hayo Kitaifa yatafanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza kuanzia Mei 2 hadi 3, huku waathirika wa ukiukwaji wa uhuru wa habari wakitazamiwa kutoa ushuhuda juu ya changamoto walizokabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

journalists

Simon Kiberege  ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Nchini Tanzania – MISA amebainisha Kauli Mbiu ya mwaka huu kuwa ni “Kupata taarifa ni haki yako ya msingi: Idai” ambapo amesema kuwa kuubana Uhuru wa Vyombo vya Habari ni kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na MISA-Tanzania, UNESCO, Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Umoja wa Mataifa Ofisi ya Tanzania, Taasisi ya Konrad-Adenauer-Stiftung Tanzania (KAS), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Klabu ya Waandishi wa Habari Mwanza na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top