Loading...

KIGOGO WA TIC ALIYESUSIA MISHAHARA MIAKA MITATU AJILIPA KWA NAMNA HII

 

Moja kati ya mambo ambayo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyasimamia kidete na kuyakemea kwa nguvu zote ni rushwa, matumizi mabaya ya rasilimali za umma na ufisadi.

Katika Awamu ya Tano ya uongozi tuliyonayo sasa  kila kiongozi amekuwa na staili yake ya kutawala; Mwalimu Nyerere alihimiza Sera ya Ujamaa akaja mzee ruksa (Ally Hassan Mwinyi) kisha mzee wa Uwazi na Ukweli (Benjamin Mkapa) pia akaja Maisha Bora kwa Kila Mtanzania (Jakaya Kikwete) na sasa mzee wa Hapa Kazi Tu John Pombe Magufuli kwa hakika tunaona mambo mengi.

Imepita miaka mitatu tangu  Juliet Rugeiyamu Kairuki achaguliwe kushika Wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambaye ni Mwanasheria mwenye Shahada ya Kwanza na ya Uzamili kwenye Sheria akiwa na utaalamu wa miradi ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi.

Julieth anadaiwa kujilipa POSHO ya zaidi ya shilingi milioni 25 kwa mwezi kwa madai ya kufidia mshahara mnono aliokuwa akilipwa huko South Afrika japokuwa ukweli halisi wa mshahara aliokuwa analipwa kabla ya kuja Tanzania ni Dola za Kimarekani 9,260 na si 15,000 kama alivyodai analijitetea Julieth.

Cha kushangaza zaidi Juliet amedaiwa kutochukua mishahara serikalini kwa takribani miaka mitatu tangu aajiriwe huku akiendelea kujineemesha kwa posho hizo jambo lililopelekea leo hii Rais Dk. Magufuli kutengua uteuzi wake kwa kile alichodai mshahara hautoshi.

Mambo haya yanatokana na Utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne uliowapa mwanya wafanyakazi wa umma uhuru mkubwa uliopelekea kufanya ufisadi wa kutisha kwa kujilimbikizia mali na kufanya matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za umma.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top