Loading...

BREAKING NEWS: WIZARA YA ARDHI IMETOA SHERIA KALI KWA MASHIRIKA YA UMMA KWA UKWEPAJI WA KULIPA KODI YA ARDHI NA KUTOA TAMKO HILI...

 

Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi inadai zaidi ya shilingi billioni 14 mashirika ya umma ambayo yameshindwa kulipa kodi ya ardhi.

Miongoni mwa mashirika yanayodaiwa ni pamoja na TANESCO, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO), Wakala wa Majengo (TBA), Shirika la Ndege Tanzania  na Makumbusho ya Taifa ambapo kama mashirika hayo yatashindwa kulipa fedha wanazodaiwa yatafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheria.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi Rehema Kilonzi ameeleza kuwa mashirika mengi yamekuwa hayalipi kodi ya pango la ardhi kwa kufikiria kuwa hayapaswi kulipa kodi ya ardhi.

“Tuna mashirika mengi tunayoyadai ambayo ni pamoja na TANESCO, Shirika la Viwango TBS, SIDO, TBA na sio haya tu yapo mengine ambayo faini zake zinakaribia milioni 800” . Alisema Rehema

Aidha wizara hiyo katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu imefanya ukaguzi katika maeneo ya Sinza na Kijitonyama na kubaini ukiukwaji wa masharti ya uendelezaji ardhi kwa kubadili matumizi yaliyoainishwa
katika miliki zao ikiwemo kugeuza maeneo ya makazi kuwa biashara

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top