Loading...

FARID MUSSA: NAAMINI NITASONGA MBELE HISPANIA

 

Winga wa Azam FC Farid Mussa ambaye yupo Madrid nchini Hispania amesema, anaamini kiwango chake cha uchezaji kitamuwezesha kusonga mbele katika majaribio nchini humo.Farid ambaye ameshafanya majaribio kwa siku tatu katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili ijulikanayo kama Segunda ya nchini Hispania amesema, katika majaribio ambayo alipewa kwa kucheza mechi alicheza vizuri na kocha alikubali kiwango chake.

Farid amesema, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa majaribio Kocha alimpa maelekezo na marekebisho kwa makosa aliyoyaona yeye na anaamini kwa uelewa pamoja na uwezo wake utaweza kumfikisha mbali.

Farid amesema, soka la Hispania lipo vizuri kwa jinsi alivyoliona kwa kipindi kifupi na katika masiha yake alikuwa na ndoto za kucheza soka la nchini Hispania.

Mara baada ya kumaliza majaribio na timu ndogo ya Tenerife, wiki ijayo anaendelea na timu kubwa ya Tenerife na baada ya hapo atapelekwa katika timu za Las Palmas au Malaga ambazo zinashiriki Ligi kuu nchini humo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top