Loading...

Naibu Spika Aendelea Kuwatesa Wapinzani Kwa Kuendelea Kuendesha Bunge Licha ya Wapinzani Kugoma Kuingia Bungeni

Kwa kawaida, Spika wa Bunge, Job Ndugai au naibu wake wanapokuwa na shughuli nyingine, huachia kiti hicho kwa wenyeviti watatu wa Bunge kuendesha vikao, lakini safari hii Dk Tulia amekuwa akiingia kila siku asubuhi na jioni.


Mei 31, mwaka huu wabunge wote wa upinzani walianza kususa vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo kwa madai ya kutokuwa na imani naye, hasa baada ya kuzuia hoja ya kufukuzwa kwa wanafunzi 7,802 katika chuo cha Udom.


Hoja hiyo iliwasilishwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari lakini Dk Tulia alisema haikuwa na umuhimu kwa wakati huo, jambo lililozua tafrani baina ya kiongozi huyo na wabunge wote wa upinzani.


Kutokana na hali hiyo, wabunge hao walipitisha azimio la kususa vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo na tangu siku hiyo, kila anapoingia bungeni kuongoza kikao wamekuwa wakitoka ukumbini.


Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye kwa sasa yuko nchini India kwa matibabu, amekuwa akisaidiwa na Dk Tulia pamoja na wenyeviti watatu wa Bunge ambao ni Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge
Tangu wabunge wa upinzani waanze kususa vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, kiongozi huyo wa Bunge ameamua ‘kukomaa’ na kiti hicho, hatua inayosababisha wapinzani wasipate fursa ya kutia mguu bungeni.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top