Zikiwa zimebaki siku tatu sawa
na saa 72 kabla ya kufungiwa kwa simu feki nchini Tanzania, Alhamisi
wiki hii na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA -Tanzania Communication
Regulation Authority), inakadiriwa simu za watu zaidi ya milioni 6
zitakwenda na maji.
Imeelezwa kuwa unapozungumzia watu zaidi
ya milioni sita maana yake yake ni zaidi ya simu feki milioni sita
kwani kuna wengine wana simu zaidi ya moja.
Kufuatia hali hiyo, Wikienda
lilizungumza na watu mbalimbali akiwemo Mbunge wa Mtera (CCM) mkoani
Dodoma, Livingstone Lusinde ambaye alisema serikali imefanya makosa kama
ilitaka udhibiti wa vitu feki basi ingedhibiti kwenye uingiaji na siyo
kujitwisha mzigo kwa dhambi ya kuwasababishia Watanzania kutumia vitu
feki.
“Kiukweli serikali ilichofanya ilifikiri
ni kama kuhamisha mfumo wa mawasiliano wa analojia kwenda digitali
lakini imekosea sana, imejitwisha mzigo mkubwa wa dhambi, kwanza
serikali itapoteza mapato lakini hata hizo kampuni na hata Watanzania
wenyewe zaidi ya milioni kama sita watapoteza mawasiliano,’’ alisema
Lusinde.
TCRA iliahidi kuzifungia simu zote feki ifikapo Juni 16, mwaka huu na hakutakuwa na muda wa nyongeza.
Post a Comment