April 30 2016 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama amekutana na waandishi wa habari Dodoma ili kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya dawa za kulevya na namna ya kukabiliana na tatizo hilii.
Waziri Mhagama pia amepiga marufuku kwa watumishi wa Hospitali zote kutowauzia dawa za Methadone waathirika wa dawa za kulevya kwakuwa ilishatangaza kuwa ni bure…>>’Tumetoa onyo kali, na kila mtoa huduma ambaye atakiuka misingi ya huduma hii atachukuliwa hatua‘
Kama wewe ni mtumiaji wa Shisha hii pia inakuhusu, Waziri Mhagama anasema..>>>’Tumeanza kufanya utafiti na tumegundua kwamba kuna kila dalili ya matumizi ya dawa za kulevya katika shisha‘
‘Niwaombe Watanzania haswa vijana wanaojihusisha katika matumizi ya shisha katika maeneo ya starehe wachukue tahadhari sana, ni eneo ambalo linapelekea matumizi ya dawa za kulevya‘
Post a Comment