Anasema redio za mikoani ndizo zimekuwa zikiwapa support bila kujali kuwa wanatoka Clouds lakini redio karibu zote za Dar zimekuwa zikibania nyimbo zao.
Diva ambaye anaandaa album yake, The Life of The Diva, amesema kuwa hicho ni kitu ambacho angependa kuona kinafutika.
“Mimi naona wako so unprofessional, mbona sisi Clouds FM watu wazuri, mimi Sam Misago kaja, katoa wimbo ataitwa kwenye XXL nyimbo yake itachezwa, sisi mbona nyimbo zetu hamchezi?” amehoji Diva.
“Nilipeleka nyimbo East Africa Radio na ina haki zote za kuchezwa na haikuchezwa kwasababu natoka Clouds Media, kwanini wanatufanyia hivi? Hii ni biashara, wao wafanye kazi zao, na sisi tufanye kazi zetu lakini when it comes to music, sisi tunafanya serious kabisa,” amesisitiza.
Post a Comment