Kutoka Bungeni Dodoma Mkutano wa bunge umeendelea tena leo April 28 2016 ambapo mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amewasilisha bungeni ripoti mpya ya tuhuma za IPTL, Tegeta Escrow pamoja na standard Bank ya Uingereza.
Katika mambo ambayo zitto ameyazungumzia ni kuhusu Takukuru na kesi za ufisadi nchini ikiwemo ya Ufisadi wa HatiFungani ya Tshs 1.2 trilioni Standard Bank ya Uingereza na Uchunguzi wa IPTL Tegeta Escrow Account, Kuhusu hatifungani ya trilioni 1.2 ya Standard Bank ya Uingereza Zitto amesema…….
>>>Waliopo mahakamani ni wanaosemekena kutumika kupeleka rushwa. Mjumbe kashtakiwa, lakini aliyemtuma hajashtakiwa na aliyepelekewa kilichotumwa hajashtakiwa. Hapa kuna tatizo la msingi ambalo tukilitatua Serikali yetu itaepuka masuala kama haya siku za usoni.
>>>Naomba tupate kauli ya Serikali kuhusu jambo hili kwani ni moja ya JIPU kubwa ambalo tunadhani Serikali inalikimbia. Serikali inaogopa nini? Serikali inamwogopa nani? Kwanini kesi ya ufisadi wa IPTL unakaliwa kimya? Kwa maslahi ya nani?
>>Katika taarifa zote ambazo TAKUKURU inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna hata siku moja wanasema kuhusu uchunguzi huu na lini wahusika waliochota fedha za umma watafikishwa mahakamani.
Post a Comment