April 17 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia baadhi ya changamoto zinazoendelea katika jiji lake ikiwa ni pamoja na vitendo vya matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na baadhi ya viongozi, Makonda anasema>>
‘Kwenye mkoa wetu wa Dar es salaam tuna mambo ambayo yamekuwa yakiendelea ambayo yamekuwa yakikiuka sheria, kanuni na taratibu, moja ya vitu vilivyobainika katika stendi ya ubungo imebainika kwamba Meneja anatumia sharia ya mwaka 2004 kulipa mapato, wakati sharia inayotambulika kwa sasa ni sharia ya mwaka 2009’
‘Mkataba wa mwaka 2009 kwa mwezi tunapaswa kukusanya si chini ya mil 84, wakati wa mwaka 2004 tunakusanya mil 42 kwa mwezi, manaake tunapoteza mil 42 kwa mwezi’
‘Hapa inamaana kwa mwaka ni zaidi ya Milioni 500 zinapotea, na ukiangalia kuanzia mwaka 2009 tumepoteza jumla ya Bil 3, ajabu waliosaini mkataba wa tarehe 30/01/2015 ndio walewale waliosaini tarehe 31/01/2015’
Lakini pia ishu ya maegesho ya magari haijampita Makonda, na anasema ‘Upande wa maegesho ya jiji inaonekana mzabuni tenda yake ilikwisha muda wake, chaajabu haikutangazwa tenda bali akaandikiwa barua ya kuongezewa muda, jambo ambalo halipo kisheria’
‘Sasa hapa inaonekana kuna uhusiano mazuri sana kati ya wanaokusanya pesa na wale wanaopokea, na watu hao ni viongozi’
Vipi kuhusu ishu ya bodaboda? Makonda anasema ‘Faini ya makosa ya pikipiki ni shilingi elfu 20, lakini Tambaza anawatoza watu elfu 80, imefika hatua wanakatazwa kumkamata mtu bila kujieleza, lakini kinachofanyika ni kinyume na taratibu’
‘Hawa Wakurugenzi ambao ambao badala ya kutusaidia sasa wameamua kutuangamiza, nimeiomba mamlaka husika ya nidhamu ichukue hatua stahiki, mimi kwenye mkoa wangu siwahitaji kuendelea kuwanyonya wana Dar es salaam’
Post a Comment