Wananchi wa Ethiopia wameeleza namna muuaji wa watu zaidi ya 182 kuwa alikuwa ameshikilia bunduki na ni raia wa Sudan Kusini upande wa Magharibi mwa Gambela mkoa wa ulioko karibu na mpakani.
Maafisa wa polisi nchini Ethiopia bado hawajawatambua washambuliaji ni akina nani? Lakini wameeleza kuwa hawana uhusiano wowote na serikali ama vikosi vya waasi nchini Sudan Kusini.
Waziri wa mawasiliano Getachew Reda ameiambia BBC kwamba vikosi vya Ethiopia walijibu mashambulizi hayo na kuwafuatilia mpaka mpakani.
Shambulio hilo la mwishoni mwa juma lililopita limegharimu maisha ya raia wasio na hatia wakiwamo akina mama na watoto. Vifo vya watu hao vimeongezeka hadi kufikia 208,idadi hii inajumuisha wale waliouawa mwezi uliopita katika maeno tofauti ya kijiji cha kebeles.
Wauaji hao hawakuishia kuwaua raia wasio na hatia bali, walipora mifugo inayokadiriwa kufikia elfu mbili serikali imetamka hayo katika waraka wake .
Serikali ya Ethiopia imekuwa ikichukua hatua kali dhidi ya washambuliaji amesema waziri wa maendeleo na uhusiano wa shirikisho na mifugo Kassa Teklebirhan wakati akizungumza na kituo cha habari cha Fana Broadcasting Corporate (FBC).
Kwa muujibu wa Kassa amesema washambuliaji hao ndio waliotekeleza mashambulizi katika vijiji vya Nare, Jikawo na Mekuwe vilivyoko katika wilaya ya Woreda ukanda unaolekea mpakani na kuingia nchini Sudan Kusini.
Jeshi la ulinzi nchini Ethiopia linajitahidi kuchukua hatua kwa kuulinda mpaka na kufanikiwa kuua wauaji 60 wa kikundi hicho na kukamata silaha kumi na moja, ikiwemo silaha aina ya machine gun.
Serikali ya Ethiopia imetoa salama za rambirambi kwa raia walio kumbwa na shambulio hilo la mwishoni mwa wiki.
Post a Comment