Imezoeleka kwamba ndoa za kikatoliki
zikifungwa zimefungwa lakini pamoja na sharti hilo idadi ya ndoa
zinazovunjika inaendelea kuongezeka ambapo sasa kanisa katoliki limekuja
na hii ya kuanzisha tuzo maalumu kwa Wanandoa wakongwe zaidi kwa mwaka
huu katika kanisa hilo.
BBC SWAHILI
wameripoti kwamba Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar es salaam limeandaa
kliniki ya ndoa ili kuweza kuwapa fursa Wanandoa kuimarisha ndoa zao
kiimani, Padre Novatus Mbaula ambaye ni mkurugenzi wa
ndoa na familia anaeleza lengo la kliniki hii ni kuwapa nafasi wanandoa
kupata neno la Mungu na kuweza kuongea juu changamoto zao mbalimbali
kuongea kuhusu maisha yao ya ndoa.
Ni nafasi ambayo wanandoa ambao wana
uzoefu mkubwa katika ndoa wanaweza kuwafaidisha wanandoa wachanga na
miongoni mwa watu waliohudhuria kliniki hii ni wanandoa wenye ndoa yenye
miaka 61, Brigedia Jenerali mstaafu Francis Mbena mwenye
umri wa miaka 86 alifunga ndoa akiwa na miaka 25 mwaka 1965
June,anasema wao zamani walikua wanafuata mtu na familia gani na ina
vigezo gani.
Walikua wanaangalia tabia kama msichana
hana tabia nzuri huoi huko, kama familia ina watu walevi bali unatafuta
familia yenye watoto wenye tabia nzuri ili na wewe uweze kupata watoto
wenye tabia nzuri.
S
Post a Comment