Ilidaiwa kuwa, katika siku za karibuni, msanii huyo alimshambulia mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Nasra lakini pia aliharibu simu yake yenye thamani ya shilingi 600,000.
Juni 6, mwaka huu, yaani Jumatatu iliyopita, Young D akiwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini hapa, aligongewa mlango na kutakiwa kutoka.
“Lakini alipotoka na kugundua ni askari na wanamtaka waende naye kituoni, alileta ujeuri kidogo, ikabidi wamkwide na kumuweka chini ya ulinzi mpaka kituoni.
“Mbaya zaidi, alikuwa hajavaa shati ni suruali tu, ikabidi aende polisi hivyohivyo. Unajua hawa wasanii wetu bwana sijui huwa wanawaza kitu gani katika ustaa wao,” kilisema chanzo kimoja kilichoshuhudia dogo huyo akiwekwa mtu kati na askari hao.
Habari zaidi zinasema kuwa, Nasra na Young D ni wapangaji wa nyumba moja lakini hawana uhusiano mzuri kwani mara kwa mara wamekuwa wakikwaruzana kwa sababu ambazo hazijulikani kirahisi.
“Siku ya tukio, inasadikiwa kuwa walikwaruzana sana, ndipo dogo (Young D) akaamua kumvaa mwanadada huyo na kumpa vitasa (ngumi) kisha kuivunja simu yake,” kiliongeza chanzo.
Katika Wabongo Fleva wanaotamba, Young D naye yumo ambapo amepata jina kupitia vibao vyake viwili, Ujanjaujanja na Kijukuu.
Askari mmoja wa Kituo cha Urafiki ambaye aliomba asiandikwe jina kwa sababu si msemaji, alipoulizwa na Amani kuhusu hatima ya mwimbaji huyo alisema: “Upelelezi unaendelea, ukikamilika atapelekwa mahakamani.”
Post a Comment