Serikali
itawafikisha Mahakama ya Kisutu leo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu na mmiliki wa gazeti lililofungiwa la Mawio, Simon Mkina kwa
kuandika habari za uchochezi.
Mkina alisema baada ya kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kuwa kwa mara ya kwanza watafikishwa mahakamani.
“Nimekuja
kama ilivyo amri kufika hapa kila siku asubuhi, ila nimeambiwa kesho (
leo ) tunatakiwa kufika mahakamani na wenzangu,” alisema Mkina.
Katika
kesi hiyo, atakuwapo pia mhariri na mwandishi wa habari iliyosababisha
kufungiwa, Jabir Idrisa pamoja na mchapishaji wa gazeti hilo.
Lissu ameunganishwa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi zilizoandikwa kwenye gazeti hilo.
Pamoja
na Gazeti la MAWIO kufungiwa Januari mwaka huu baada ya kudaiwa
kuandika habari za uchochezi zilizohusu mgogoro wa kisiasa visiwani
Zanzibar ikiwa na kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Z’bar’ katika toleo
lake la 182 la Januari 14-20, 2016, bado serikali inawang’ang’ania.
Akizungumza na wanahabari Mkina alilaumu kitendo cha polisi kukamata hadi watoa maoni wa gazeti.
Post a Comment