Ujauzito huo ni wa aliyekuwa mumewe, Sadifa Juma, mbunge wa Jimbo la Donge, Visiwani Zanzibar ambapo kitendo cha mimba hiyo kuwa ya mbunge, kimemsumbua Wastara hadi kuamua kuondoka ili akapate muda mzuri wa kutafakari nchini Msumbiji.
Taarifa kutoka kwa vyanzo, zinaeleza kuwa Wastara alipoondoka nchini, aliwaaga baadhi ya mastaa wenzake kuwa anakwenda kufuata biashara zake za nguo nchini humo lakini Risasi Jumamosi lilichimba na kupata ubuyu ulionyooka kuwa aliondoka nchini kwa ajili ya kwenda kutafakari ujauzito huo.
NDUGU AVUJISHA UBUYU KAMILI
Ndugu wa karibu na Wastara ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazeti, amefunguka kuwa baada ya Wastara kuachika, aligundua ni mjamzito hivyo alichanganyikiwa na kuamua kwenda Msumbiji kwa ajili ya kutafakari zaidi ujauzito huo.
“Hakuwa na jinsi kwani akiangalia alishatoka kwa mwanaume, angewezaje kumwambia kuwa ana ujauzito wake? Akaamua kukimbilia huko kwa ajili ya kujipanga ingawa anavyoonekana anatamani amzalie mbunge huyo,” alisema ndugu huyo.
NDUGU AZIDI KUTIRIRIKA
Ndugu huyo alizidi kushusha ‘vesi’ kuwa mimba ya Wastara inasadikiwa kuwa na miezi miwili au mitatu kwani tangu aachane na mumewe huyo, alikuwa akiumwaumwa na wakati mwingine alikuwa akitapika hovyo ambapo mwanzo alificha lakini yalipomfika shingoni alifunguka.
“Alitufichaficha lakini baadaye akawa hana jinsi, akaona atueleze na sisi tumemshauri tu aende akapumzike na ajiandae kutuletea kiumbe kipya,” alisema ndugu huyo.
Baada ya habari hiyo kutua Risasi Jumamosi, Wastara alitafutwa kwa njia ya simu ya mkononi, akafunguka:
“Dah! Sijui niseme nini, kiukweli watu wanaongea sana, nimeondoka nchini kwa shughuli zangu binafsi lakini maneno ni mengi, wewe si wa kwanza kunipigia simu. Sikutaka kuongea kabisa juu ya masuala yangu ya ndoa iliyopita wala maisha yangu kwa jumla.”
Risasi Jumamosi: Kwa nini unaongea hivyo wewe funguka swali nililokuuliza, una ujauzito au la?
Wastara: Ndiyo, kwani cha ajabu ni nini? Yule niliyekuwa nalala naye si shangazi yangu, kila mtu anajua niliolewa na aliyenioa (Sadifa) wala si mjomba wangu.
TUJIKUMBUSHE
Wastara aliachika Aprili, mwaka huu baada ya kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Juma ambapo ndoa yao ilidumu kwa muda kwa miezi mitatu tu na kuvunjika.
GPL
Post a Comment