KESI ya Emmanuel Masonga, aliyekukuwa mgombe ubunge katika Jimbo la Njombe Kusini (Chadema) itatolewa uamuzi tarehe 9 Mei mwaka huu, anaandika Wolfram Mwalongo.
Akizungumza na Mwanahalisi Online, Masonga amesema, alifungua madai dhidi ya Eluminata Mwenda, Mkurugenzi wa Uchaguzi katika jimbo hilo na Edward Mwalongo, mbunge wa jimbo hilo kwa madai ya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa. Kesi hiyo kesi hiyo namba 6 ipo mbele ya Jaji Jacob Mwambegele.
Masonga alidai, uchaguzi huo uligubikwa na rushwa, matumizi mabaya ya magari ya serikali kwa shughuli za chama na kwamba, tayari ameikabidhi mahakama vielelezo vyake na kinachosubiriwa ni uamuzi.
Masonga amewataka wananchi kuwa na utulifu wakati huu na kwamba, ataendelea kutoa ushirikiano kadhi atakavyoweza.
Post a Comment