Watu 16 wameuawa katika mji mkuu wa Mirsi, Cairo, baada ya bomu kulipuliwa kwenye mgahawa mmoja, ripoti zinasema.
Shambulio hilo limetokea katika eneo la Agouza, katikati mwa jiji hilo.
Gazeti la The Cairo Post linasema watu watatu waliokuwa wamejifunika nyuso zao walirusha bomu mgahawani na kisha kutoroka.
Shirika la habari la Reuters limemnukuu afisa mmoja wa usalama, ambaye hakutajwa jina lake, akisema mmoja wa washukiwa ni mfanyakazi wa zamani wa mgahawa huo.
Mgawaha huo ulikuwa ghorofa ya chini ya ardhi kwenye jengo hilo, jambo lililoifanya vigumu kwa watu kutoroka.
Wahasiriwa walifariki kutokana na majeraha ya moto au kwa kutokana na moshi. Watu watano wamejeruhiwa.
Mji wa Cairo umeshambuliwa mara kadha na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu.
Juhudi za wanamgambo hao wa Kiislamu zilizidi baada ya kung’olewa mamlakani kwa Rais Mohammed Morsi mwaka 2013.
Post a Comment