Loading...

BREAKING NEWS: AGIZO LA MAGUFULI NGOMA NZITO

 
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati 2,600 kwa shule za msingi 74 za umma wilayani humo, Mkurugenzi wa manispaa hiyo, John Wanga, alisema wilaya hiyo ina upungufu huo wa madawati na kwamba uongozi uko katika jitihada za kuhakikisha inakamilisha kwa wakati uliopangwa.
“Tatizo kubwa liko kwa shule za msingi ambazo zina wanafunzi 78, 227. Upande wa shule za sekondari tunao upungufu wa madawati 4,812 na haya 2,600 ndiyo yako tayari kwa ajili ya kukabidhiwa kwa shule husika,” alisema Wanga.
Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wanatekeleza agizo la Rais kwa wakati, halmashauri inaendelea kuhamasisha wadau kwa ajili ya kutengeneza na kukamilisha kabla ya mwisho wa muda uliowekwa.
Kutokana na uharaka wa mahitaji ya madawati hayo, wilaya ya Ilemela iliamua kuratibu utengenezaji huo katika shule ya ufundi ya wavulana Bwiru na madawati hayo yanatengenezwa na wanafunzi kwa kushirikiana na mafundi kutoka nje ya shule.
“Kila dawati linatugharimu Shilingi 98,000 mpaka 100,000 ambapo vifaa na mahitaji yote yananunuliwa na uongozi wa Halmashauri. Wanaotengeneza ni shule na wao hutudai Sh. 15,000 kwa kila dawati,” alisema.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Manju Msambya alisema ametoa agizo kwa watendaji wote kukataza matumizi ya vifaa vya shule kinyume cha maelekezo ili kulinda miundombinu ya shule na kuwaomba wazazi wasipotoshwe kuhusu kuchangia maendeleo ya kitaaluma kwa watoto wao na shule kwa ujumla.
Alisema wilaya inatarajia kuandaa hafla ya uchangiaji wa madawati kwa kuwahamsisha wazazi katika kukamilisha kazi hiyo kwa kuwa asilimia kubwa ya fedha za kutengeneza madawati ni za mapato ya ndani ya halmashauri.
Naye Msitahiki Meya wa Halmashuri ya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga alisema madawati 2,600 yaliyokabidhiwa jana, yanatarajiwa kusambazwa kwenye shule 74 za msingi za umma wilayani na kata 19 za wilaya hiyo zinatarajiwa kupata madawati 139 kila moja.
“Tunaendelea kukarabati madawati, meza, na viti vibovu katika shule za msingi na sekondari na mpaka sasa madawati 799 katika shule za msingi yameshakarabatiwa na meza 1,358, viti 1,237 vinaendelea kukarabatiwa katika shule za sekondari,” alisema Mulunga

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top