Loading...

HABARI KUBWA:.TRENI YAFANYA YAKE, ABIRIA 1000 WAKUTWA NA JANGA ZITO NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HUKO DODOMA

Abiria wa treni ya reli ya kati wakisubiri treni yao iendengamae ili waendelee na safari ya Kigoma
ABIRIA zaidi ya 1000 waliyokuwa wakisafiri na treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), jana wamekwama mkoani Dodoma na kushindwa kuendelea na safari kutokana kuanguka treni ya mizigo kati ya Kituo cha Itigi na Kitakaa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Tukio la kukwama abiria hao limetokea jana saa 2:00 asubuhi mjini hapa mara baada treni hiyo ya abiria ilivyo kuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Tabora, Kigoma na Mwanza kuzuiwa na Mkuu wa Kituo cha Dodoma.
Akizungumza na wandishi wa habari mjini hapa Mkuu wa Kituo hicho cha Dodoma, Suzo Kazimoto, amesema uongozi wa TRL umemalizika kuzuia kuendelea kwa safari ya abiria hao kutokana kuelezwa mapema kuwa huko waliko kuwa wakielekea kumetokea ajali.
Amesema baada ya kupata taarifa ya kuanguka treni hiyo wameona ni vema kuzuia katika kituo hicho kwa vile abiria hao wangeweza kupata huduma zote za kijamii zinazohitajika baadala ya kuiruhusu kwani huenda wangeenda kwamba katika eneo ambalo halina huduma hizo muhimu.
“Taarifa tulizonazo ni kwamba mafundi wako kwenye eneo wanaendelea na kazi ya kurejesha na tumewatangazia abiria wetu kuwa safari yao itaendelea kuanzia saa 12:00 jioni leo,” amesema Kazimoto.
Akizungumzia malalamiko ya abiria kwamba baadhi yao walikuwa hawana fedha za kujikimu, Kazimoto, amesema wakati huo walikuwa wakikusanya idadi halali ya abiria wenye tiketi ili aweze kufanya mawasiliano na Makao Makuu Dar es Salaam kwa ajili ya kupata kibali cha kuwapatia abiria hao fedha ya kujikimu.
“Hata kama leo, ni nusu siku kwamba benki zinafungwa mapema hilo siyo tatizo tutaangalia kilichopo ili tuweze kuwa saidia abiria wetu,” amesema Kazimoto.
Awali baadhi ya abiria walilalamikia uongozi wa Shirika hilo kushindwa kujenga njia mbili tangu walipokabidhiwa reli hiyo na mkoloni kwani kama kungekuwa na njia mbili kama ilivyo katika nchi nyingine safari yao ingeendelea bila mvutano kama huo.
mmoja wa abiria hao, Khadija Salum ambaye alikuwa akielekea Kigoma huku akiwa na mtoto mdogo alikuwa akilia njaa baada ya kuibiwa Sh. 70,000 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kujikimu wakati wa safari hiyo.
Pia, amesema kuwa baada ya kukwama katika kituo hicho baadhi ya wafanya biashara walipandisha bei za bidhaa ghafla hivyo kuwaongezea ugumu katika kumudu kununua bidhaa hizo ikiwemo maji ya kunywa na chakula.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top