Loading...

‘Vyeti viwe na sifa nje ya mipaka’

Jengo la Chuo Kikuu huria (OUT) Kanda ya MbeyaSERIKALI imevitaka Vyuo Vikuu vyote nchini kuhakikisha vyeti wanavyotoa katika fani zote vinakuwa na sifa ya kutambulika kitaifa na kimataifa, anaandika Christina Haule.
Lengo ni kuwafanya wahitimu kukubalika kwa viwango sawa vilivyopo duniani jambo litakalosaidia kuingiza Watanzania kwenye ajira za kikanda na kimataifa.
Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amesema hayo jana kwenye siku ya wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe iliyokwenda sambamba na harambee ya kuchangia bweni la wanafunzi wa kike katika chuo hicho.
Samia amewataka kuendela kuhakikisha kuwa, viwango na sifa za kitaaluma vya wahitimu katika ngazi na fani mbalimbali ikiwemo shahada, stashada, uzamili na uzamivu vinakuwa na sifa ya kutambulika kokote duniani.
“Isiwe kwamba mhitimu wetu napovuka mipaka yetu ya nchi hadhi ya shahada yetu ni sawa na Diploma kwingineko,” amesema Samia.
Hata hivyo alizitaka taasisi za elimu kusaidia kuweka mazingira wezeshi ya kujiajiri “ipo haja kuhuisha vigezo na utaratibu wa kuhakiki, kusimamia na kupima utekelezaji wa mitaala yetu ili kuhakikisha kwamba idadi ya wataalamu tunaozalisha wanakuwa na ujuzi wa juu.”
Prof. Josehat Itika, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho amesema, jumla ya Sh. 4.5 bilioni zinahitajika ili kuweza kujenga bweni hilo la wanafunzi wa kike litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 900.
Amesema katika kuboresha mundombinu ya chuo hicho na kampasi zake, jumla Sh. 40 bilioni zinahitajika.
Hata hivyo ameiomba serikali kukamilisha azma yake kwa kutenga kiasi cha Sh. 15 bilioni ili kurejesha kituo kitakachofundisha maadili ya uongozi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top