Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Baraza hilo na kusainiwa na Dk Adolf Rutayuga Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ilisema Baraza linatoa fursa hiyo ya pekee kuanzia tarehe 23 mpaka tarehe 27 mwezi huu ambayo ni wiki ya utumishi wa umma nchini.Taarifa hiyo imeeleza kwamba, Baraza katika kipindi hicho kitapokea mrejesho juu ya utendaji wake na changamoto mbali mbali ambazo wadau wa elimu wanakutana nazo wanapota kupata huduma kutoka NACTE.
Zoezi hili litafanyika kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa nane mchana katika jengo la udahili NACTE makao makuu lililopo eneom la viwanda vidogo Mikocheni jijini Dar es Salaam jirani na Chuo Cha Kodi jijini Dar es Salaam. Kwa wale waliopo mikoani huduma hiyo itatolewa katika ofisi zetu za kanda,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilitaja ofisi za kanda zitakazopokea mrejesho ni pamoja na zile zilizopo mikoa ya Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Tabora, Mwanza na Zanzibar.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zitolewazo na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki.
Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za uendeshaji mafunzo ili tuzo zitolewazo na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
Post a Comment