Loading...

BREAKING NEWS..WAZIRI MKUU AJIUZULU

 David Cameron, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika Muungano wa Ulaya (EU), anaandika Pendo Omary.
Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo ang’atuke.
Waziri Mkuu huyo aliongoza kampeni ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.
Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.
Sauti yake iliibua hisia hasa aliposena naipenda sana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda huo wote.
Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.
Cameron akiwa ameandamana na mkewe amesema bila shaka sasa utawala mpya unahitajika utakaoweza kutathmini mbinu na mkataba wa kujiondoa kutoka kwa muungano huo wa bara Ulaya.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top