Hivi
karibuni taarifa hizo zilieleza kuwa utafiti uliofanywa na Tamisemi
umebaini kuwapo kwa ziada ya walimu 7,988 wa masomo ya sanaa na biashara
hivyo haitaajiri walimu hao badala wataajiri wa masomo sayansi na
hisabati.
Akizungumza
na wanahabari Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mhandisi Mussa Iyombe amewataka
wananchi kupuuza taarifa hizo kwani hazina ukweli wowote na zinalenga
kugombanisha,kujenga chuki kati ya Serikali na walimu wa masomo hayo.
"Siyo
kwamba ajira za walimu hakuna, ajira zipo. Ila wakati ukifika
tutawangazia tunachosubiri sasa hivi suala la bajeti kuu liishe
kwanza," amesema Mhandisi Iyombe.
Post a Comment