Loading...

Zitto Kabwe: Kwa Hili la Rais Kuendesha Bunge Kwa Remote Control Tutampinga Kwa Nguvu Zote

Mhe. Zitto Kabwe aliandika haya kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema hawatakubali kuona wanarudishwa nyuma au kuona misingi ya taasisi za uwajibikaji zikibomolewa.
"Rais Magufuli tunakuunga mkono kwa dhati kupambana dhidi ya ufisadi. Tunakupinga kwa nguvu zote kupambana dhidi ya demokrasia. Kuanzia mwanzo tumekuunga mkono dhidi ya ukwepaji kodi, ubadhirifu, uvivu na uzembe. Tangia mwanzo tulionya kuwa ni lazima udhibitiwe na Bunge ili ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba. Hivi sasa wewe Rais ndio unaendesha Bunge kwa remote control. Tutakupinga kuturudisha nyuma. Hutafanikiwa kamwe kubomoa misingi ya taasisi za uwajibikaji tulizoanza kuzijenga". Alisema Zitto Kabwe.

Mbali na hilo Zitto Kabwe alisema Tanzania inataka uongozi madhubuti na siyo utawala wa imla na kudai watanzania hawatakubali kurudi nyuma katika utawala wa imla.

"Narudia nukuu muhimu sana " ukitaka kutawala tawala peke yako. Ukitaka kuongoza ongoza na wenzako". Rais Magufuli Tanzania inataka Uongozi madhubuti na sio utawala wa imla. Huko tumeshatoka na Watanzania hawatakubali kurudi huko". Aliongeza Zitto Kabwe

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top