Loading...

BUNGENI KUMENOGA MBUNGE WA CCM "GOODLUCK MLINGA" AMTOA BUNGENI WAZIRI WA ARIDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, WILIMU LUKUVI

 
Jana alilazimika kumtoa Bungeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi, kwenda naye katika Kijiji cha Chikutu, wilayani Ulanga kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa kijiji hicho na mwekezaji.
Mgogoro huo uliokuwa ukifukuta kwa muda mrefu, unatokana na wananchi wa kijiji hicho kutaka kupewa eneo la hekari 49,025, linalomilikiwa na Kampuni ya Tanzania Nuthelds Limited, inayotaka kuendesha kilimo cha kalanga miti. Zao hilo lilishindwa kuendelezwa tangu walipopatiwa mwaka 1988.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika kijiji hicho, Mlinga, alisema ameamua kumleta Waziri Lukuvi kwa kuwa yeye ndiyo mwenye dhamana ya ardhi.
Alisema wakati wa kampeni zake za uchaguzi wa kuwania nafasi ya ubunge mwaka jana, alikutaka mgogoro huo na kuwaahidi wakimchagua atahakikisha anaumaliza na kupata mwafaka.
“Ndugu zangu wana Chikuti, wakati wa kampeni nilipokuja hapa mlinambia hili tatizo la shamba, nikasema nichagueni nitamleta waziri husika na leo nimekuja na Waziri Lukuvi hapa nimemtoa Bungeni kuja kulimaliza nashukuru nimetimiza ahadi yangu,” alisema.
Katika taarifa yao ya uongozi wa kijiji, iliyosomwa na Mwenyekiti Justus Nalionga, alimueleza Waziri Lukuvi kuwa mwekezaji huyo tangu alipopatiwa eneo hilo hajaendeleza na sasa idadi ya wananchi katika kijiji hicho imeongezeka na wengi wao hawana maeneo ya kilimo hivyo wanaomba kupatiwa eneo hilo.
Waziri Lukuvi alisema eneo hilo alipewa kihalali mwekezaji huyo kwa masharti ya kuendesha kilimo na ujenzi wa kiwanda hicho cha kalanga miti na kutoa ajira kwa wananchi wa kijiji hicho pamoja na kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii.
Alisema licha ya mwekezaji huyo kulipa kodi, lakini ameshindwa kuendeleza kotokana na sababu mbalimbali ikiwamo miundombinu na hivi sasa ameamua kuanza rasmi uwekezaji wa kiwanda hicho baada ya miundombinu kutengenezwa.
Waziri Lukuvi alisema, kutokana na kuchelewa huko kwa mwekezaji, ameamua kumpiga penati kwa kumnyanganya hekari 9,025 na kwapatia wananchi kila kaya ili walime kilimo hicho na kukiuzia kiwanda, huku mwekezeji akibakiwa na hekari 40,000.
“Huyo mbunge wenu kanitoa kweli Dodoma kuja kumaliza mgogoro huu, huyo mwekezaji yupo kihalali kabisa, alishindwa kuendeleza kutokana na sababu mbalimbali, amenihakikishia sasa anaanza ujenzi wa kiwanda pamoja na kupanda kalanga miti, sasa mimi nampiga penati hizi hekari 9,025 namnyang’anya nawapeni nyinyi, lakini nataka mlime kilimo hicho cha kalanga miti na soko lake lipo hapa kwa mwekezaji,” alisema Lukuvi na kushangiliwa.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Luise Gota, alisema wamechelewa kuendeleza kutokana na ucheleweshaji wa daraja lilokuwa linajengwa na serikali ambalo kwa sasa limekamilika na muda wowote wataanza.
Alisema kwa kuanzia wanatarajia kupanda miche 10,000 ya kalanga miti ambayo mingine watawapatia wananchi bure na utalaamu wa kilimo hicho na kisha kuanza ujenzi wa kiwanda na kutoa ajira kwa wakazi wa kijiji hicho.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top