Loading...

Zari Anasa Ujauzito Tena!

Hii ni habari ya motomoto kabisa! Mama la mama, Zarinah Hassan ‘Zari The  Boss Lady’ amedaiwa kunasa ujauzito wa mpenzi wake, Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Risasi Mchanganyiko lina ubuyu ulionyooka.

Taarifa hizo za ndani ya familia zimevuja ikiwa ni takriban miezi nane tangu mrembo huyo ampe jeuri Diamond ya kutembea kifua mbele kwa kumzalia Tiffah ambapo inaelezwa kuwa, amefanya hivyo makusudi kuwakata ‘vilimilimi wabaya’ wake.Zarimond


TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kutoka ndani ya familia ya Wasafi Classic Baby (WCB), juzikati kilinyetisha kuwa, gumzo la mjini kwa sasa ni wadau wa burudani kujadili ujauzito wa Zari, ambao unaonekana kuwatisha karibia wapambe wote wa timu pinzani.
“Naomba nikudokeze juu ya Zari kuwa mjamzito tena, habari hii ni ya uhakika na kila mtu WCB anajua, Zari amenyaka mimba na cha ajabu amekataa katakata kuichomoa kama Diamond alivyokuwa akimshawishi.

NDIYO CHANZO CHA UGOMVI
“Huwezi kuamini ugomvi wote ambao umekuwa ukidaiwa kuendelea kati ya Diamond na Zari umesababishwa na ujauzito huo ambapo Diamond amekuwa akitumia nguvu nyingi kumuomba Zari achomoe mimba hiyo lakini hakuna hata siku moja ambayo ameonesha dalili za kumuelewa.

MIMBA INA MIEZI MINNE
Chanzo hicho kilizidi kuweka bayana kuwa, kinachomsikitisha Diamond ni kwamba, mimba hiyo inazidi kukua jambo ambalo anaona si sahihi kwa sasa kwani ana mtoto (Tiffah) ambaye bado hajatimiza hata mwaka mmoja.
“Jamaa anaona soo, anaona kama jamii haitamuelewa hivi, jitihada zake za kumshawishi zinagonga ukuta na mbaya zaidi mimba kwa sasa ina kitu kama miezi minne,” kilisema chanzo hicho makini.

SAFARI ZA SAUZ ZATAJWA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, safari ambazo Diamond alikuwa akizifanya mara kwa mara kwenda Afrika Kusini  (Sauz), nyingi zilikuwa ni za kutatua mgogoro huo ambao umeikumba familia ya WCB, kiasi kwamba hadi wazazi wote wameshirikishwa lakini mwisho wa siku hakuna muafaka.
“Si unakumbuka kuna kipindi Diamond alikuwa anakwenda Sauz mara kwa mara, ishu hiyo ndiyo ilikuwa inampeleka lakini hazikuzaa matunda, mamaa kagoma,” kilisema chanzo hicho.

FAMILIA YAKE YAMSHANGAA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, familia yake imemshangaa Diamond kwa nini hakuwa makini wakati alijua kabisa Tiffah bado angali mdogo.
“Wamemshangaa sana kwa kushindwa kuwa makini wakati kwa sasa kuna mbinu nyingi sana za kuepuka ujauzito, sasa matokeo yake amesababisha hadi kuwe na mvutano unaokosa muafaka,” kilisema chanzo hicho.

NDUGU WA DIAMOND ATHIBITISHA
Mwanahabari wetu alipokuwa akiichimba habari hii, alizungumza na mmoja wa ndugu wa Diamond ambaye alikiri kuwa Zari ni mjamzito lakini akaombwa asitajwe jina maana suala hilo limegubikwa na usiri mzito.
“Ndiyo hivyo kama ulivyosikia. Zari hataki kutoa, nahisi kwa sababu ya kuwakomesha zile timu pinzani lakini anashindwa kujua upande wa pili familia inashindwa kukubaliana naye maana ni jambo la aibu kupata mimba kabla mtoto wa awali hajafikisha hata mwaka,” alisema ndugu huyo.

MSIKIE DIAMOND
Baada ya kupenyezewa ubuyu  huo wa motomoto, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Diamond mwenyewe ili aweze kuweka bayana habari hiyo ya heri, ambapo hakutaka kukataa wala kukubali licha ya kukiri kuzisikia habari hizo.
“Dah! Habari hizi sijui muda mwingine huwa mnazinyaka vipi, sijui hapa niseme nini zaidi ila unachotakiwa kufahamu mimi bado nahitaji kupata watoto zaidi ya mmoja na ifahamike kuwa ninapenda watoto sana, maana uwezo wa kuwahudumia ninao hata hivyo kushika mimba kwa Zari ni mapema sana,” alisema Diamond.

MAMA YAKE NAYE
Mama mzazi wa msanii huyo, Sanura alitafutwa ili kusikia maoni yake, lakini badala yake, aliishia kucheka na kumuomba mwandishi wa habari hizi kuachana na mambo hayo.

Chanzo:Global Publishers

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top