Upande wa viwandani kuna mtambo mmoja wa Kiwira ndio unazalisha umeme,Vile vile viwandani unatumika kwenye viwanda vya saruji Tanga, Mbeya, kile cha karatasi kilichopo Mgololo na cha Dangote kilichoko Mtwara.
Katika hili nasikitika sana kwa Dangote Kuwa JIPU la kutisha nchini, Wanamkataba TANCOAL kila mwezi Tani 13,500 cha kushangaza tangu kiwanda hiki kimefunguliwa wamenunua Tani 2000 tu,Wanaingiza Makaa ya Mawe toka Afrika kusini na November mwaka jana waliingiza Tani 45,000, Agent akafanya manuva wakaclea mizigo kwa provision clearance wakapewa siku 14 kulipa VAT ama kupeleka msamaha wa kodi amabao kwa taarifa tu walishawahi kupewa na TIC lakini hadi leo daa siku kumi na nne hazijaisha, hawajalipa na hivi sasa Meli ya Makaa ya Mawe yenye Tani 36,000 kutoka Afika Kusini na na Nyingine ya Gypysum Tani 36,000 kutoka Oman bila kibali cha Importation kutoka Wizara husika Nishati na madini,Nasasa wanashinikiza mzigo ushuke Daaa!!
Ukakasi huu na hujuma mbaya kwa Taifa vinaifanya Dangote kuwa moja ya majipu ya kutisha wakisaidiwa na mzawa mwenzetu KAZIMOTO wa Pale PTA akisaidiwa na Wahindi kadhaa na wazawa wengine Majipu.
Nakumbuka Waziri Muhongo alifanya ziara nchi nzima na kuwatambua wachimbaji wadogo wenyeuwezo wa kuzalisha mamilioni ya Madini haya, aliwataka waunde umoja na aliagiza Makampuni haya kununua Madini haya kutoka kwa wazawa kuzalisha ajira na Faida kwa Taifa na alienda Mbali zaidi na kutukumbusha kwamba haya madini yanaubora kuliko madini hayo kwa kiwango kikubwa,TBS sinauhakika juu yenu kwa hili maana sina uhakika kama ukaguzi wa ubora wa bidhaa kwa yale ya November
Je ni kweli Ubora wa Dangote na ahadi zenye neema kwa nchi hasa mikoa ya kusini ndiyo hiyo,Najiuliza juu ya wakala mzawa kuwatetea wawekezaji juu ya kutolipa VAT Jipu hili ni ukakasi kwa Serikali ya Magufuli maana siku mbili tu alipopokea kijiti Amiri jeshi wetu mkuu pale Wizara ya Fedha alifoka kutotoa misamaha ya kodi lakini nakumbuka mwaka jana Bunge letu tukufu lilifuta utoaji misamaha ya VAT kwa wawekezaji wote wa TIC,hawa wawekezaji nchi zote walizowekeza wanalipa Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na wanauwezo wa kulipa.
Gypysum inapatikana kwa wingi pale Lindi inakuwaje wanaagiza kutoka Oman,nawaita Takukuru kuchunguza Majipu ya mawakala wa namna hii,What about our National interest?
Hata hivyo moja ya Dangote kujengwa Mtwara ni matumizi ya Gesi yetu asilia,kupata pesa na kusaidia ajira Ukakasi unaikumba Dangote upande wa ajira pia kunaunyanyasaji na rushwa ya kutisha kupata ajira vinavyo fanywa na HR(Chapalwa).
Takukuru nendeni Pale ni aibu kwa Taifa,Kapwapwa na HR Chapalwa anatumika katika kuwawahujumu waliokosa vigezo kupata ajira ndani ya kiwanda wafunga Tulubai za magari yanayopakia Sementi wanakatwa posho zao malalamiko yako hadi kwa Wenyeviti wa maeneo husika yanayozunguka Majirani wa Aliko Dangote.
Udereva unatoa laki 3 na wafunga turubai wako katika vikundi wanatozwa 5000 kwa kila Lori linapolipa ujira wake wa 15,000 kufungiwa ikumbukwe Kiwanda kinauwezo wa kuzalisha kwa siku Tani 7500 hata kuingiza zaidi ya Maroli 500 kwa siku. Mmoja wa Wenyeviti analalamika anasema Toka wakati wa ujezi HR huyu amehujumu wananchi wetu wengi ni aibu hapa mtu huyu,uliza dada yoyote hapa atakupa sifa zake,Wizi wa Mafuta uliokithiri vinatia doa nchi yetu kwa wawekezaji. Serikali ya Tanzania ilitoa msamaha wa kodi lita zaidi ya milioni 2 kwa Dangote wizi huu kwa siku unaihujumu Dangote lita 1000 kila siku unafanywa na wazawa washirika wa HR Takukuru Mpoo????
Pongezi za dhati kwa Waziri wa Fedha kwa kulinda maslahi ya Taifa na Pongezi Prof. Muhongo kwa kuthamini wachimbaji na kusimamia Taratibu, Sheria na Maslahi mapana ya Taifa Letu baada ya kubaini Jipu hili la Dangote na kuchukua hatua kali dhidi ya hujuma hii kwa Taifa. Sisi Wazawa wachimbaji wadogo wadogo tuko pamoja nanyi tutapigania haki na maslahi ya Taifa letu Tunapongeza juhudi za Rais wetu katika Vita dhidi ya Rushwa, ubadhirifu vilivyolitafuna Taifa letu kwa kiwango kikubwa.
Post a Comment