Ishu za
wanafunzi vyuoni kufukuzwa na migomo zimezidi kuchukua headlines ambapo
baada ya UDOM na UDSM, taarifa niliyoipata ni kutokea Kilombero, Ifakara
kwenye chuo kikuu kishiriki cha tiba na afya cha St. Fransis.
Taarifa
hiyo inasema wanafunzi wapatao 134 wa mwaka wa tatu wa shahada ya
udaktari 134 hawajaingia madarasani kwa takribani wiki kadhaa ambapo
mmoja wa wanafunzi hao amezungumza na millardayo.com na kueleza haya madai baada ya kasoro mbalimbali kujitokeza kwenye matokeo yao ya muhula wa tano……
>>>Utawala
umesema haya mambo yatawezekana lakini kwa sababu utawala wamekuwa na
ahadi nyingi hewa wanafunzi tumeona ili tuweze kuendelea na masomo
inabidi tujiridhishe na matokeo yetu ya mwisho ya muhula wa tano kama
yako vizuri ili tuendelee na muhula wa sita na hapo mvutano ndio
ukaanza.
Post a Comment