ALIYEKUWA
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Tunus Mgaya
amesema amesikitishwa na taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya habari
za kukosoa maamuzi ya serikali ya kuwasimamisha kazi kuwa hayakuzingatia
sheria na kanuni zilizowekwa.
Mgaya
ambaye hakuwa tayari kueleza kama taratibu za kusimamishwa kwao
zilifuata utaratibu au la, amewataka waandishi wa habari kuwa na vyanzo
vya uhakika katika habari zao.
“Mimi
nikiwa miongoni mwa watendaji waliopumzishwa kazi, napenda kueleza kuwa
sihusiki na taarifa hizo, suala hili limeshapita na kutolewa uamuzi na
serikali na tuiache Tume iendelee kufanya kazi,” alisema Profesa Mgaya alipozungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kukabidhi ofisi.
Aidha,
Profesa Mgaya aliweka wazi kuwa, anaunga mkono jitihada za Rais John
Magufuli katika kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata elimu
ya msingi bure na kutolewa kwa elimu inayokidhi viwango stahiki kitaifa
na kimataifa na kusema jambo hilo ni jema na linapaswa kuungwa mkono kwa
nguvu zote.
Katika
hatua nyingine, alimtaka Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi ,
Profesa Joyce Ndalichako kuendeleza jitihada za kuinua ubora wa elimu
katika ngazi zote ili kuwa na taifa lenye watu walioelimika vizuri na
lenye mchango mkubwa katika kuendeleza taifa.
Post a Comment