Loading...

BREAKING NEWS: HABARI YAKUSIKITISHA SANA, RAIS MAGUFULI AWANYOOSHA TENA WANAFUNZI 7,802 WALIOTIMULIWA UDOM NA PIA AMETOA KAULI HII NZITO

 DK. John Magufuli, Rais wa Tanzania
RAIS John Magufuli amefunga mjadala kuhusu wanafunzi waliotimuliwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), anaandika Charles William.
Amesema walistahili kutimuliwa. Wanafunzi hao 7,802 walikuwa wa ngazi ya stashahada UDOM, serikali iliwaondoa kwa madai ya kutostahili kuwepo chuoni hapo.
Rais Magufuli amesema hayo leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alipohutubia wanafunzi wa chuo hicho baada ya kumaliza shughuli kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa utakaogharimu zaidi ya Dola za Marekani 40 milioni.
“Nimezungumza na Profesa Idrisa Kikula, (Makamu Mkuu wa chuo UDOM) ameniambia kuwa, baadhi ya wanafunzi waliondolewa UDOM hawakustahili kusoma diploma kwani hawakuwa na sifa.
“Ilikuwa lazima wapitie certificate, na amesema yeye alilazimishwa kuwapokea wanafunzi hao. Je, angegoma afukuzwe kazi,” amehoji na akiongeza;
“Nilikuwa nawasubiria na wanafunzi wa degree wa UDOM wagome, nao wote wangeondoka!”
Rais Magufuli amewashangaa wanaoilaumu serikali kwa hatua ilizochukua na kusema, “wanasiasa wanasema, tumewaondoa wanafunzi kwa ghafla na wamekosa pa kulala lakini hakuna lolote ‘it’s nonsense’ (ni upuuzi), kwani lazima tuweke maslahi ya taifa mbele na tuache siasa.
“Haiwezekani fedha za serikali ziache kufanya kazi ya kutoa mikopo kwa waliofaulu na ziende kwa vilaza waliofeli kidato cha nne.”
Kuhusu hatma ya wanafunzi waliokuwa wamefaulu Kidato cha Nne lakini serikali iliwapeleka UDOM ili kusoma stashahada maalum za ualimu wa masomo ya sayansi na sasa wamefukuzwa, Rais Magufuli amesema, amemuagiza Waziri wa elimu Profesa Joyce Ndalichako apitie ile orodha yao.
Na kwamba, na achukue wale waliofaulu ili aangalie namna ya kuwapeleka shule lakini wale waliofeli watafute wenyewe vyuo vinavyolingana na ufaulu wao.
Katika hotuba hiyo iliyolazimu utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusimamisha ratiba za masomo kwa masaa sita ili kuwapa nafasi wanafunzi kusikiliza hotuba ya Rais, Profesa Rwekaza Mkandara, Makamu Mkuu wa Chuo hicho alimuomba Rais Magufuli kushughulikia tatizo la mabweni kwani ni kero kubwa kuliko zote kwa wanafunzi wa chuo hicho.
“Mheshimiwa Rais, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanakabiliwa na kero kubwa tatu,
Tatizo la kwanza ni uhaba wa mabweni, tatizo la pili ni uhaba wa mabweni na tatizoa tatu ni uhaba wa mabweni ya wanafunzi,” amesema Profesa Mkandara.
Akijibu madai hayo, Rais Magufuli amesema yupo tayari kuunga mkono ujenzi wa mabweni ya wanafunzi kwani ni jambo la muhimu.
“Ikiwa wawekezaji wa Mlimani City wanachangia bilioni 1.3 kila mwaka, na nimekuliza matumizi yake bahati nzuri umeelezea vyema, naomba sasa kwa kuongeza na fedha zingine nitakazotoa tengeni eneo ujenzi wa bweni ndani ya eneo la chuo hikihiki, mimi nitatafuta bilioni 10 za kuwaongeza na tangazeni tenda ujenzi uanze hata kesho,” amesisitiza.
Katika ziara hiyo chuoni hapo Rais Magufuli aliongozana na Mkuu wa Chuo hicho  ambaye pia ni Rais Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu, Gharib Bilali na Ally Salum Hapi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright KAZI YANGU | Designed By AFROPIXELS MEDIA CO. LTD
Back To Top